Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amefanya ziara ya kikazi ya Ukaguzi na Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Kipindi cha Julai hadi Septemba 2023 Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Vijijini.
Senyamule amefanya ziara hiyo tarehe 20 Oktoba 2023 na kuzungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri hiyo na kusisitiza kila Halmashauri kuhakikisha inavuka malengo ya makusanyo katika bajeti iliyotengwa ili utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyopangwa ikamilike kwa wakati na kwa ubora.
Ameagiza watumishi kutimiza wajibu wao na kufanya kazi kwa weledi na ufanisi katika utekelezaji na usimamizi wa mradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo.
"Tunasisitiza ukusanyaji wa mapato kwa kuwa kila sekta imeguswa kwa upande wake, hivyo kila mmoja katika kipande alichopewa ahakikishe anachangia katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwakuwa mchango wa kila mmoja ni muhimu na ni jukumu letu sote katika kuongeza mapato katika maeneo yetu”
Senyamule amesisitiza.“Kila mtu ajione ni sehemu ya upatikanaji wa mapato simbo zuri kuona wataalamu wanashindwa kufukisha baadhi ya fedha zilizopangwa kwa kila Halmashauri tunatamani tuone mapato yanaongezeka kwa wingi” Amesema Senyamule.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi amesema suala la kuimarisha ukusanyaji wa mapato ni wajibu wa kila mmoja na kusisitiza kuwa bila kuwepo kwa mapato uendeshaji wa Halmashauri unakua ni mgumu sana.
“Kila kitu tusimamie kwa weledi na ufanisi ili tufike katika kila mipango tuliyojiwekea katika Halmashauri yetu ili kufikia malengo katika ukusanyaji wa mapato tuliyopangiwa na kuhakikisha kila mmoja anasimamia wajibu wake ili kufanikisha dhamira yetu.” Amesisitiza Dkt. Mkanachi.
Katika ziara hiyo pia, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amekagua miradi ya ujenzi wa Nyumba ya Mkurungezi ambayo fedha ilitoka Shilingi Milioni za 150,nyumba za watumishi shilingi Milioni 80, Jengo la Ofisi ya Halmashauri, Shuleni ya Msingi Isabe ambapo fedha kiasi cha shilingi Milioni 80 zimetolewa kwaajili ya ujenzi wa madarasa 03, Ofisi O1 na jengo la Computa 01 na Hospitali ya Wilaya ya Kondoa ilipokea Milioni 750 kwaajili ya ujenzi uliopo katika kijiji cha Bukulu kata ya Soera Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
No comments:
Post a Comment