Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari (TPA) Plasduce Mbossa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPA Mhe. Balozi Ernest Mangu wakitia saini Mkataba wa Uendeshaji wa Gati namba 4 mpaka 7 za Bandari ya Dar es Salaam kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari (TPA) Plasduce Mbossa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPA Mhe. Balozi Ernest Mangu wakitia saini Mkataba wa upangishaji wa Gati namba 4 mpaka 7 za Bandari ya Dar es Salaam pamoja baina ya Kampuni ya DP World ya Dubai iliyowakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Sultan Ahmed bin Sulayem kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2023.
Viongozi mbalimbali pamoja na wageni waliohudhuria hafla ya Utiaji saini Uwekezaji na Uendeshaji wa Sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali kwenye hafla ya Utiaji saini Uwekezaji na Uendeshaji wa Sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2023.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Makame Mbarawa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Godius Kahyarara wakitia saini Mkataba wa Nchi Mwenyeji baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya DP World ya Dubai iliyowakilishwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Sultan Ahmed bin Sulayem kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2023.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Makame Mbarawa akipongezana na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Sultan Ahmed bin Sulayem mara baada ya kusaini Mkataba wa Nchi Mwenyeji baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya DP World ya Dubai kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2023.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Mikataba ya Uwekezaji wa Bandari iliyosainiwa imezingatia maoni yaliyotolewa kupitia makundi mbalimbali ya kijamii, pamoja na
sheria na taratibu zote za nchi.
Rais Samia amesema hayo leo wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba 3 ya uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), serikali na Kampuni ya DP World ya Dubai iliyofanyika Ikulu, Chamwino.
Aidha, Rais Samia amesema serikali ilisikiliza maoni mbalimbali yaliyotolewa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, vyama vya Siasa, asasi za kiraia, wanaharakati, vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, viongozi wa dini na baadhi ya viongozi wastaafu.
Vile vile Rais Samia amesema mikataba iliyosainiwa imetokana na makubaliano ya awali kati ya serikali na Mamlaka ya Dubai ambao wameridhia mahitaji na matakwa ya nchi kama yalivyoainishwa kwa kuzingatia maslahi ya taifa.
Mikataba iliyosainiwa ni Mkataba wa Nchi Mwenyeji (Host Government Agreement); Mkataba wa Upangishaji Ardhi (Lease Agreement) na Mkataba wa Uendeshaji wa Bandari (Concession Agreement).
Rais Samia pia amesema uimarishwaji utakaofanywa kupitia uwekezaji huu utakuza biashara za ndani na nje, pamoja na kuwezesha shughuli za kiuchumi za nchi jirani hivyo kuongeza mapato ya serikali na kukuza uchumi wa taifa.
Mikataba hii 3 imesainiwa kwa kuzingatia Kifungu cha 2 cha Sheria ya Ubia Namba 6 ya mwaka 2023 (the Public Private Partnership Act Cap 103) na Kifungu cha 2 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma Namba 5 ya mwaka 2023 (the Public Procurement Act No 5 of 2023).
No comments:
Post a Comment