October 16, 2023

KLINIKI YA ARDHI DODOMA YAANZA KWA MAFANIKIO









Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.Ally S.Gugu ameshiriki zoezi la Kliniki ya Ardhi lililoongozwa na Wataalamu kutoka Divisheni ya Uendelezaji wa Makao Makuu ya kuhudumia wananchi kwaajili ya kutatua cahngamoto mbalimbali za Ardhi.

Kliniki ya ardhi imeanza rasmi leo tarehe 16 Oktoba 2023 na inatarajia kuisha tarehe 20 Oktoba 2023 katika Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya zamani kuanzia saa3:00 Asubuh hadi 1:00 jion.

Kliniki ya Ardhi itahusisha utoaji wa hati,Utoaji wa Elimu ya masuala ya Ardhi Pamoja na ulipaji kodi ya pango la Ardhi.

No comments:

Post a Comment