October 06, 2023

KAMANDA MALLYA ASHANGAZWA NA WANAFUNZI 121 KUTOMALIZA KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARI BARA-MBOZI-SONGWE.

Kamanda a Polisi mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya ameshangazwa na taarifa ya wanafunzi 121 wa Sekondari ya Kutwa ya Bara kuto maliza kidato cha nne.

ACP Mallya aliyasema hayo Oktoba 05, 2023 akiwa katika mahafali ya shule ya sekondari Bara na kukemea mambo ambayo yanafanya wanafunzi kuto maliza shule.

Wahitimu 81 tu ndio waliofanikiwa kuhitimu kidato cha nne kati ya wanafunzi 202 walioanza kidato cha kwanza mwaka 2020.

"Mambo ambayo yanafanya wanafunzi kutokumaliza shule kama wazazi kuwa walevi wa kupindukia, kuamini imani za kishirikina, kuwaruhusu watoto kwenda kufanya kazi za majumbani, kuwaruhusu wanafunzi kwenda kwenye shughuli za uchimbaji wa madini wilayani Chunya, tamaa ya mali ikiwa ni pamoja na kuwafanyia ukatili kama ukatili wa kingono na vipigo," alisema ACP Mallya.

Aidha, Kamanda Mallya aliwasihi wazazi na wananchi walioudhuria mahafali hayo kuacha mara moja vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto kwani hawataweza kukwepa mkono wa sheria.

Naye Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Dkt. Sister Shitindi kutoka Mkoa wa Kipolisi Kinondoni akiwa kama mgeni rasmi katika mahafali hayo alitoa kiasi cha shilingi Laki 5 kwa ajili ya kununua Printer na vifaa vya michezo ili kuwezesha shughuli za kitaaluma shuleni hapo na kujenga afya ya akili na mwili kupitia michezo kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Sambamba na hayo wazazi, walimu na wanafunzi wamelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa kuendelea kushirikiana na wananchi katika suala la utoaji elimu kuhusu ukatili na usalama wa raia na mali zao.Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Dkt. Sister Shitindi kutoka Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambaye ndiye mgeni rasmi katika mahafali hayo akizungumza. ASP Dkt. Sister Shitindi kutoka Mkoa wa Kipolisi Kinondoni akiwa kama mgeni rasmi katika mahafali hayo alitoa kiasi cha shilingi Laki 5 kwa ajili ya kununua Printer na vifaa vya michezo ili kuwezesha shughuli za kitaaluma shuleni hapo na kujenga afya ya akili na mwili kupitia michezo kwa wanafunzi wa shule hiyo.

No comments:

Post a Comment