Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Myovizi na kuwataka kutokupokea zawadi kutoka kwa watu wasio wafahamu ili kuepukana na janga la ugonjwa wa ukimwi au kufanyiwa kitendo chochote cha ukatili.
Matukio mbalimbali pichani yakimuonesha Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Myovizi na kuwataka kutokupokea zawadi kutoka kwa watu wasio wafahamu ili kuepukana na janga la ugonjwa wa ukimwi au kufanyiwa kitendo chochote cha ukatili.

Kamanda Mallya ameyasema hayo Oktoba 03, 2023 wakati akitoa elimu ya Ushirikishwaji Jamii katika kata ya Mahenje wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Ambapo amewaasa wanafunzi hao kuacha kurubuniwa kupitia lifti wanazopewa na vijana wanaoendesha pikipiki maarufu bodaboda ikiwa ni pamoja na zawadi kama chips vinapelekea wao kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi ingali bado ni wanafunzi na kupelekea kupoteza malengo katika masomo yao.
Aidha, walimu na wanafunzi wamelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa kuendelea kushirikiana na wananchi katika suala la utoaji elimu kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto pamoja na usalama wa mali zao.

No comments:
Post a Comment