October 23, 2023

CHEMBA WAPONGEZWA KWA ONGEZEKO LA MAPATO






Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema ili Halmashauri ya Wilaya ya Chemba iendelee katika ukusanyaji kwa mapato ni lazima kufuatilia kwa makini vyanzo vyote vilivyopo ndani ya Wilaya hiyo.

Ameyasema hayo leo tarehe 23 Oktoba 2023 wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi ya kutathmini, kukagua na kufanya ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Kipindi cha Julai hadi Septemba 2023.

“Niwapongeze kwa kufanya vizuri kwenye kusimia miradi na ongezeko la mapato Katika Wilaya ya Chemba ni vizuri kwenda kwa kasi hiyo na kila mtu afanye kwa ngazi ya Idara ili kuleta mabadiiliko zaidi kwa kila sekta" 

“ Kila baada ya Miezi mitatu kutakuwa na mambo ya ufuatiliaji wa mapato ili kuona Kwanini miradi mingine imekuwa changamoto kwa mapato ya Halmashauri” amesema Senyamule.

Pia amesisitiza suala la utunzaji wa mazingira katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kila Afisa mazingira kuhamasisha wananchi kuhusu suala la utunzaji wa mazingira 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bi. Prosister Tairo amesema katika mwaka wa Fedha 2023/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba imepanga kukusanya na kutumia kiasi cha fedha cha Shilingi Bilioni 28.7  na katika kipindi cha robo ya kwanza Julai hadi Septemba Halmashauri ilipanga kukusanya Shilingi Bilioni  7.1 kutoka katika vyanzo vyote vya mapato.

“Hadi kufikia Septemba 2023 Halmashauri imekusanya Bilioni 7.4 sawa na asilimia 103 ambapo kwa kipindi cha Julai  hadi Septemba Jumla ya Shilingi Bilioni 5.3 zimetumika ”amesema Bi. Tairo.

No comments:

Post a Comment