September 29, 2023

TUME YA MADINI YAANZA VYEMA KATIKA MICHEZO YA SHIMIWI





Tume ya Madini  imeanza vizuri katika Mashindano ya  Shirikisho la Michezo ya Wizara, Taasisi na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea katika viwanja vya Chuo cha Mkwawa mkoani Iringa ambapo katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya wanawake ya Tume ya Madini imeibuka mshindi dhidi ya timu ya wanawake ya Wizara ya Utamaduni na Michezo baada ya kushinda kwa pointi 1-0.

Akizungumza baada ya ushindi huo , Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Tume ya Madini, Azihar Kashakara amesema siri ya ushindi katika michezo ya SHIMIWI ni mazoezi na nidhamu ya hali ya juu na kuongeza kuwa wamejipanga katika kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo yote ikiwa ni pamoja na kuvuta kamba, mpira  wa miguu, riadha n.k

Katika hatua nyingine  amesema kuwa sambamba na kutumia mashindano hayo kuimarisha mahusiano na Taasisi nyingine za Serikali, watatumia kutangaza  fursa na mafanikio katika Sekta ya Madini, majukumu ya Tume ya Madini na Dira ya Madini ya mwaka 2030 inayosema " Madini ni Maisha na Utajiri"

No comments:

Post a Comment