Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko akihutubia wakati alipofungua kongamano la pili la wiki ya kitaifa ya Ufutailiaji na Tathmini lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko akimkabidhi tuzo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Kongamano la pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufutailiaji na Tathmini lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akitoa salamu wakati wa Kongamano la pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufutailiaji na Tathmini lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko alipotembelea Banda la Idara ya Menejimenti ya Maaafa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu wakati Kongamano la pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufutailiaji na Tathmini lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko akiwa na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuhutubia Kongamano la pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufutailiaji na Tathmini lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko akimkabidhi tuzo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Kongamano la pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufutailiaji na Tathmini lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akitoa salamu wakati wa Kongamano la pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufutailiaji na Tathmini lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko alipotembelea Banda la Idara ya Menejimenti ya Maaafa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu wakati Kongamano la pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufutailiaji na Tathmini lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
*************
Na Mwandishi wetu - ArushaNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko amesema kama Serikali haitafanya Tathmini ya Shughuli zake haitakuwa na uwezo wa kujipima na vihatarishi vya utekelezaji wa mipango yake.
Kutokana na umuhimu huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia
Suluhu Hassan anasisistiza Serikali kuwa na Uratibu wa shughuli zake.
“Unaweza kukuta Serikali za
Mitaa na Serikali kuu kila mtu anafanya jambo lake hakuna vinavyosomana,
tujifanyie tathmini ili tusije kuwa watu wa kuduwaa kunini hili limetokeaje.”
Alisisitiza
Dkt.Biteko aliongeza kusema
kuwa asiyejifanyia tathmini atakuwa ni mtu wa hasara hivyo kujifanyia tathmini
kunaifanya serikali kubaini matatizo mapema na kuweza kuyatafutia ufumbuzi
kabla hayajaleta hasara. Dkt. Biteko ametoa wito kwa washiiriki wa kongamano
hilo hasa watendaji wa serikali kufanya ufuatiliaji na tathmini bila kuweka
mbele rasilimali fedha.
Sambamba na hilo, Naibu Waziri
Mkuu Dkt. BITEKO amewataka maafisa masuhuli wote nchini kuviwezesha vitengo vya
ufuatiliaji na tathmini katika wizara na taasisi zao kwa kuhakikisha kunakuwa
na wataalamu wa kutosha, vitendea kazi na rasilimali fedha ili viweze
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulika na masuala ya (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.
Jenista Mhagama amesema, wakati kongamano hili likifanyika kwa mara ya Pili
hapa nchini, Serikali imefanyia kazi kwa Asilimia mia, (100%) utekelezwaji wa
agizo la uanzishwaji wa Idara za Ufuatilijaia na Tathmini katika Wizara na
Serikali.
Awali akiongea wakati wa
Ufunguzi wa Kongamano hilo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na
Uratibu) Dkt. Jim Yonazi, alisema kwa kufuatilia mwendeno wa utekelezaji wa
kujipima matokeo, Taasisi za Umma zinaweza kujihakikishia kuwa zipo katika njia
sahihi za utekelezaji katika kufikia malengo yake, hivyo Ufuatiliaji na Tathmini
ni njia nzuri ya kujifunza na kuwajibika.

No comments:
Post a Comment