Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2020 kutoka kwa Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage, katika halfla
iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Agosti 21,2021. Rais aliipongeza Tume
kwa kuratibu na kusimamia uchaguzi huo Mkuu wa mwaka 2020 kwa ufanisi mkuu.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa (Mst) Semestocles Kaijage akisoma
taarifa kwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya kukabidhi Ripoti ya
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam, Agosti 21,2021.
Makamishna
wa Tume na wageni mbalimbali waalikwa wakifutailia hafla ya kukabidhi ripoti ya
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 iliytokabidhiwa
kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam, Agosti 21,2021.
Mhe. Rais Samia amesema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage.
Amesema katika uchaguzi huo wagombea wa nafasi ya Urais na Makamu wa Rais walikuwa 30, kati yao wanawake walikuwa 7, katika ngazi ya ubunge wagombea walikuwa 1,257 kati yao wanawake walikuwa 293 na kwenye ngazi ya udiwani wanawake walikuwa 668 kati ya wagombea 9,231.
Pia, Mhe. Rais Samia ametoa wito kwa wanawake kujiamini na kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika siasa ili waweze kupata fursa ya kuingia katika vyombo vya maamuzi.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Samia amevipongeza vyama vya siasa vilivyoshiriki katika hafla hiyo kwa kusema kuwa uwepo wao umethibitisha ukomavu wa kisiasa na demokrasia nchini.
Mhe. Rais ameitaka Tume ya
uchaguzi (NEC) kulinda haki za wagombea kwa kuziangalia upya sheria zinazosimamia
uchaguzi kwa kuhakikisha kwamba
Watanzania hawakosi haki ya kugombea kwa kwa makosa madogo madogo.
Halikadhalika, Mhe. Rais Samia amehimiza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika michakato ya uchaguzi. Hii ni kwasababu shughuli nyingi duniani kwasasa ikiwemo masuala ya uchaguzi yanafanyika kwa njia hiyo ili kupunguza malalamiko ya wagombea na kuharakisha utoaji wa matokeo kwenye ngazi zote.
Hafla ya makabidhiano ya Taarifa hiyo ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleimani Abdulla, na viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, dini na Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza baada ya kupokea Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 wa Urais, Ubunge na Udiwani. Hafla ya kukabidhi ripoti hiyo ilifabyika , Ikulu jijini Dar es Salaam, Agosti 21,2021.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amevitaka vyama vya siasa kuwapa nafasi
wagombea Wanawake katika uchaguzi mkuu ujao kwasababu wana ushiriki mkubwa
katika uchaguzi ikilinganishwa na wanaume.
Mhe. Rais Samia amesema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage.
Amesema katika uchaguzi huo wagombea wa nafasi ya Urais na Makamu wa Rais walikuwa 30, kati yao wanawake walikuwa 7, katika ngazi ya ubunge wagombea walikuwa 1,257 kati yao wanawake walikuwa 293 na kwenye ngazi ya udiwani wanawake walikuwa 668 kati ya wagombea 9,231.
Pia, Mhe. Rais Samia ametoa wito kwa wanawake kujiamini na kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika siasa ili waweze kupata fursa ya kuingia katika vyombo vya maamuzi.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Samia amevipongeza vyama vya siasa vilivyoshiriki katika hafla hiyo kwa kusema kuwa uwepo wao umethibitisha ukomavu wa kisiasa na demokrasia nchini.
Halikadhalika, Mhe. Rais Samia amehimiza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika michakato ya uchaguzi. Hii ni kwasababu shughuli nyingi duniani kwasasa ikiwemo masuala ya uchaguzi yanafanyika kwa njia hiyo ili kupunguza malalamiko ya wagombea na kuharakisha utoaji wa matokeo kwenye ngazi zote.
Hafla ya makabidhiano ya Taarifa hiyo ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleimani Abdulla, na viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, dini na Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
Viongozi mbalimbali walihudhuria hafla hiyo yua kukabidhi ripoti ya Uchaguzi kwa Rais

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Rufaa (Mst), Mbarouk Salim Mbarouk na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Dk. Wilson Mahera Charles wakifuatilia hutuba ya Rais.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo (kushoto) akiwa kwenye hafla hiyo.
Wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia hotuba.

Viongozi wa Juu wa Serikali wakifuatilia hafla ya kukabidhi Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.Picha mbalimbali za pamoja .
No comments:
Post a Comment