Maalim Hassan Yahya Hussein akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo , kuhusu utabiri wake wa mambo mbalimbali yatakayotokea mwaka huu.
Baadhi ya mabo aliyotabiri ni;Kutatokea kashfa kubwa sana ya ngono \au fumanizi itakayowahusu viongozi wa dini, siasa na wasanii maarufu itakayosababisha viongozi hao kufedheheshwa na kuanguka kabisa katika tasnia zao.
Mwaka huu pia kutakuwa na vifo vya viongozi wakubwa maarufu wa kisiasa na kidini, kufa ghafla vifo hivyo vitatokana na msongo wa moyo na shinikizo la damu.
Mioto mingi mikubwa itatokea nchini na duniani.
Viongozi wakubwa wa upinzani duniani na Tanzania kurejea kwenye vyama walivyovihama.
Vifo vya vya ghafla vya wasanii maarufu duniani ikiwemo Tanzania vinaweza vikatokana na fumanizi kuuliwa au kuana wenyewe.
Wimbi kubwa la vifo viliwakumba wanahabari duniani 2016 vitaendelea mwaka huu Ajali nyingi kuwakuta wanasiasa, watawala na viongozi wa dini katika mwaka huu. Source: Kamanda wa Matukio Blog.
No comments:
Post a Comment