Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka
jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja
ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara tu alipoweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja
ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa ndani ya moja ya nyumba hizo 252 mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba hizo za Shirika la
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar
ikiwa moja
ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia
ramani ya ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya
maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.
Pichani
ni Nyumba za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii Zanzibar (ZSSF) zitakazokuwa na nyumba 252, Viwanja vya Michezo kwa
Watoto,Sehemu ya kuogelea na Ukumbi mkubwa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwasalimia wananchi waliojitokeza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la
ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya
miaka 53 ya Mapinduzi.
Sehemu ya Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Hassan Suluhu
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akfurahia jambo na wanafunzi waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi la
ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya
miaka 53 ya Mapinduzi.
***********
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Samia Suluhu Hassan ameuagiza
uongozi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) uchangamkie fursa za uwekezaji wa
ujenzi wa nyumba za makazi Tanzania Bara hasa kwenye Makao Makuu ya nchi Dodoma
hatua ambayo itauwezesha mfuko huo kuongeza maradufu mtaji wake kwa uuzaji wa
nyumba hizo.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anaweka jiwe la msingi katika
mradi mkubwa wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi katika eneo la MBWENI kisiwani
Unguja ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa
Rais amesema kutokana na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na mfuko huo wa ZSSF hasa
ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi ni muhimu kwa mfuko huo kuangalia namna
bora ya kwenda kuwekeza katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara kutokana maeneo
mengi kuwa na mahitaji makubwa ya nyumba za makazi.
Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan amesema ujenzi wa nyumba za makazi Tanzania Zanzibar ulitokana na
fikra na ahadi za hayati mzee Karume kupitia ASP wakati wa haraka za kudai
uhuru za kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora ya kuishi katika kisiwa cha Pemba
na Unguja kutokana na idadi kubwa ya wananchi katika kipindi hicho kuishi
katika mazingira yasiyoridhisha.
“Miradi yote hii ni katika kuenzi
utekelezaji wa kauli ya Mapinduzi Daima yanayotaka kuleta maendeleo
yanayoonekana kwa wananchi kila uchao hususani kipindi hiki tunapotimiza miaka
53 ya Mapinduzi yetu ya Matukufu ya Zanzibar”
Makamu wa
Rais pia amewahimiza wananchi wote wachangamkie fursa za kununua na kumiliki nyumba
kwa bei nafuu na zenye miundombinu ya kisasa na huduma zote za kijamii ikiwemo
viwanja vya michezo.
Kuhusu umiliki wa nyumba kwa
Watanzania wanaoishi nje ya nchi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan ameziagiza Wizara zinazoshughulika na masuala ya ardhi Tanzania
Bara na Zanzibar kutoa ufafanuzi au tafsiri sahihi ya sheria zinazoongoza
masuala ya ardhi na umiliki wa nyumba ili kuondoa sintofahamu iliyopo kuhusu
wana diaspora kumiliki nyumba.
Amesisitiza
kuwa Serikali zote mbili zimekuwa zikisisitiza wana diaspora kuchangia
maendeleo ya nchi na kutumia fursa mbalimbali zilizoko nyumbani ikiwemo kununua
nyumba zinazojengwa na mifuko na mashirika mbalimbali hivyo ni muhimu kwa
wizara zinazoshughulikia masuala ya ardhi kutoa maelekezo haraka ili kuondoa
sintofahamu iliyopo kwa sasa kuhusu wana diaspora kulimiki nyumba kwa ajili ya
makazi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni muda muafaka sasa hivi kwa mifuko hiyo kuwekeza
katika sekta ya viwanda hasa kwenye miradi yenye tija kwani viwanda vitatoa
fursa kwa vijana wengi kuajiriwa na kuongeza kipato na kuongeza huduma za
kijamii na kupunguza umaskini kwa wananchi.
Kwa upande
wake, Waziri wa Fedha na Mipngo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Khalid
Salum Mohamed amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Serikali hiyo inaendelea kumuezi
Mzee Karume kwa vitendo kwa kujenga nyumba
za makazi na kukarabati nyumba
zilizopo ili kuhakikisha wananchi katika Kisiwa cha Pemba na Unguja wanapata
makazi bora ya kuishi.
No comments:
Post a Comment