December 09, 2016

WANANCHI DODOMA MJINI WAANZA KUPIMWA MACHO BUREE DESEMBA 9-12 MWAKA HUU

Madaktari Bingwa wa Macho wakiendelea kuwachunguza wakazi wa mji wa Dodoma iliyoratibiwa kwa pamoja kati ya  Taasisi ya Bilal Muslim Mission na Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni aibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde na kuanza leo Desemba 9-12, 2016 katika Shule ya Darul Muslemeen ambapo mpaka sasa hivi mchana wamejitokeza wananchi 3224.
 Zoezi la huduma ya macho linaendelea katika Shule ya Darul Muslemeen ambapo zaidi ya wananchi 3,224 walijitokeza katika siku ya kwanza kupatiwa matibabu hayo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mavunde, wananchi wanafanyiwa uchunguzi wa mafya na walio na matatizo wanapatiwa miwani, dawa, ushauri.

Aidha katika siku hiyo kwanza wananchi zaidi ya 100 wameanza kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

"Nawashukuru sana wananchi wa Dodoma kwa kujitokeza kwa wingi sana kushiriki katika huduma hii ambayo ni ya bure isiyo na gharama yoyote iliyoratibiwa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Taasisi ya Bilal Muslim Mission,"alisema Mavunde.

Aidha ametoa shukrani kwa wadau mbalimbali akiwepo Mbunge wa Chalinze, Ridhwan Kikwete kwa kusaidia kufanikisha utoaji wa huduma hiyo.
 Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni aibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde, akizungumza na wakazi wa Dodoma waliojitokeza kupima macho.
Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni aibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Dodoma waliojitokeza kupatiwa huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment