December 20, 2016

RAIS NA MWENYEKITI CCM DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AZUNGUMZA NA VIONGOZI 3 WA CCM ALIOWATEUA KARIBUNI

Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori  (kushoto) pamoja na viongozi wapya wa CCM aliowateua hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa  Kanali Ngemela Eslom Lubinga na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo walipoenda kujitambulisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori akishuhudiwa na viongozi wapya wa CCM aliowateua hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa  Kanali Ngemela Eslom Lubinga na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo walipoenda kujitambulisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori  (kushoto) akibadilishana mawasiliano na  na viongozi wapya wa CCM walioteuliwa hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo  na Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa  Kanali Ngemela Eslom Lubinga  walipoenda kujitambulisha kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016.
******************
Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 20 Desemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi watatu wa CCM aliowateua hivi karibuni kujaza nafasi wazi katika safu ya uongozi wa chama ngazi ya taifa.

 Viongozi hao ni Naibu Katibu Mkuu Bara Bw. Rodrick Mpogolo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Bw. Humphrey Polepole na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Siasa na Mambo ya Nje Kanali Mstaafu Ngemela Eslom Lubinga.

 Baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Bw. Humphrey Polepole amesema lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kumweleza Mwenyekiti wa CCM fikra na mipango ya awali na namna walivyojipanga kwa kushirikiana na viongozi wengine wa chama, kusimamia na kutekeleza ajenda ya mageuzi ndani ya chama ambayo msingi wake ni kuirejesha CCM kwa watu.

 "Na Mhe. Rais ametuhakikishia kwa asilimia 100 kwamba msimamo wa kufanya mageuzi kwenye Chama Cha Mapinduzi, kukirudisha kwenye misingi ambayo chama hiki kilianzishwa, yaani chama cha wanyonge na chama ambacho kinajinasibu na shida za watu, unatekelezwa.

 "Ametuambia tukafanye kazi kwa bidii, Watanzania wana matumaini makubwa sana na Chama Cha Mapinduzi na sisi tumemhakikisha kwenda kuchapa kazi ili dhamira ya kujenga Tanzania mpya iweze kuakisiwa na kuletwa na CCM Mpya" amesema Bw. Polepole.

No comments:

Post a Comment