December 07, 2016

POLISI KIGOMA WANASA RISASI 408 ZA SMG ZIKIWA NDANI YA NGUO



Na Father Kidevu Blog- Kigoma
JESHI la polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kukamata risasi 408 za bunduki  zilizo kuwa zikimilikiwa na Mtu mmoja ambaye jina lake halikutajwa mkazi wa Kijiji cha Makere Wilayani kasulu Mkoani Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jana Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma,DCP Fredinand Mtui alisema mnamo tarehe 5Desemba majira ya 08:20 huko maeneo ya makere Center katika kijiji cha Makere askari wakiwa doria walipokea taarifa kutoka kwa raia wema wanao chukia uhalifu kuwa kuna mtu wana wasiwasi nae kuwa anamzigo usio kuwa wa kawaida.

Mtui alisema Askari walianza ufuataliaji na kufanikiwa kukamata mtuhumiwa mmoja ambaye jina lake limehifashiwa kwa shughuli za kiusalama, alipo fanyiwa upekuzi mtuhumiwa huyokatika Sanduku lake  alilokuwa amebeba alikutwa akiwa na risasi 408 za bunduki aina ya SMG/SAR  alizokuwa amezifunga ndani ya nguo zake .

Aidha Mtui alisema upelelezi bado unaendelea ,Mtuhumiwa atapelekwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria pindi upelelezi utakapo kamilika  ilikutoa fundiaho kwa wananchi wengine wanao nunua siraha kwa lengo la kufanyia uhalifu. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
"nichukue fursa hii kuwaasa wahalifu wanao jihusisha na biashara ya kuuza na kununua risasi na siraha nyingine waache biashara hiyo, wafanye kazi nyingine ambazo zinatambulika kisheria vyombo vya ulinzi na usalama viko imara kuwatafuta wahalifu hao na kuwachukulia hatua za kisheria,"alisema Mtui.

Sambamba na tukio hilo alisema mnamo tarehe 6Desemba huko maeneo ya Mwanga Vamia Manispaa ya Kigoma ujiji Hussen Athuman (36) Mkazi wa mwanga Vamia alikutwa chumbani kwake akiwa  amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani.

Mtui alisema usiku wa tarehe5 marehemu alimpigia simu Dada yake  na kudai kuwa  walikuwa na ugomvi na mkewe ugomvi huo uliopelekea mkewe kuondoka  siku nne zilizo pita , na kumwambia amueleze kaka yake kwamba atachukua maamuzi magumu.

Alisema chanzo cha kujinyonga ni ugomvi baina ya baina ya marehemu na mkewe, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospital ya rufaa maweni  kusubili kukabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.                                             

No comments:

Post a Comment