December 31, 2016

MBUNGE NA MADIWANI SITA WA CCM KASULU WAADHIBIWA NA CHAMA KWA KUCHOCHEA MGOGORO


Na FK Blog Kigoma,
KAMATI ya usalama na maadili na kamati ya siasa ya Wailaya ya Kasulu imetoa adhabu kwa Mbunge wa Viti maalumu wa Mkoa wa kigoma,Josephin Ngezabuke  na madiwani sita wa Halmashauri ya mji wa Kasulu kwa tuhuma za kuchochea mgogoro wa madiwani kumpinga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu kwamba aondolewe hafai.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Kasulu Masoud Kitowe alisema kumekuwa na mgogoro Mkubwa uliodumu kwa miezi mitano  wa Baadhi ya madiwani wa Act na CCM waliomuandikia barua Mkurugenzi ya kudai Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kasulu aondolewe hafai na Chama Cha mapinduzi hakikupatiwa barua hiyo ambayo ingeweza kuwasaidia kujua chanzo cha tatizo nini.

Alisema katika mgogoro huo Madiwani wa CCM walio shiriki ni watano na kati ya hao mmoja ambaye ni Seleman diwani wa kata ya Kumnyika  amepewa adhabu ya  kalipio ambayo ataitumikia kwa miezi 18 kwa kosa na kushiriki kuandika barua ya kumkataa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo wakati jambo hilo bado halijajadiliwa katika Kikao cha Chama kwamujibu  sisi kama chama tulipo pata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi tuliwaita madiwani walio husika na kupewa onyo.

Aidha Kitowe alisema madiwani wanne waliojiorodhesha kwenye barua ya kushiriki kumpinga Mwenyekiti huyo kamati ya siasa pia imetoa adhabu ambayo kwa Mujibu wa Sheria za Chama cha Mapinduzi hairuhusiwi kuitangaza hazarani nao watsitumikia adhabu hiyo kwa miezi 12.

Alisema Madiwani hao walipohojiwa walikiri mgogoro huo una chochewa na baadhi ya watu ambao  ni Diwani wa Kata ya Murusi Steward Zinduse ambae alikuwa akigombea nafasi ya Mwenyekiyi wa halmashauri akashindwa  pamoja na  Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Kigoma Josephini Ngezabuke nao pia wamepewa adhabu ambayo hairuhusiwi kitangazwa kwa mujibu wa sheria  na barua walishapewa zinazo elezea adhabu zao.

Hata hivyo Kitowe alitaja sababu zinazo pelekea Mbunge huyo kumkataa Mwenyekiti wa halmashuri  ni kwamba aliwahi kumuomba meya wa kasulu ashiriki vikao vya halmashauri ya Mji wa Kasulu baada ya kukataliwa kwakuwa ni mjumbe wa Baraza la madiwani kakonko alijenga chuki na Mwenyekiti huyo ,jambo la pili alimuomba mea amuite Everina diwani wa viti maalumu kwa madai avuliwe madaraka ya udiwani viti maalumu kutokana na migogoro ya kifamilia kati yake na diwani huyo wa viti maalum.

"Kwa Mbunge wetu huyu migogoro ni kawaida yake ukiona Kasulu kuna migogoro ujue kuna watu wanaochochea,  ikumbukwe Mwaka 2010 kamati ya Siasa ya Mkoa ilimpa azabu ya karipio mbunge huyo kutokana na migogoro kwakuwa yeye anadai anawatu juu watatengua adhabu hiyo ndio maana anaendelea na migogoro hiyo inayo pelekea Halmashauri kushindwa kufanya Shughuri za maendeleo suala ambalo hatulifurahii sisi kama Chama.

Alisema Madiwani hao watano baada ya kupewa adhabu waliachana na mgogoro huo lakini mpaka sasa Mbunge huyo pamoja na Diwani wa Kata ya Murusi alie kosa nafasi hiyo bado wanaendeleza Mgogoro huo suala ambalo halina masilahi katika chama zaidi ya kudhohofisha halmashauri yetu ya Mji wa Kasulu.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalumu Josephin Ngezabuke alisema hawezi kwenda kwenye halmashauri ya kasulu  kuingia kwenye kikao  na kufanya vurugu kwakuwa sheria ninazifahamu ninauwezwa kufanya vurugu hata nikiwa nje siwezi kupiga kura sehemu mbili yeye ni Mjumbe wa Halmashauri ya kakonko anacho hitaji ni yeye kupewa heshima kama Mbunge wa Mkoa anapo fika katika Halmashauri ya Wilaya ya kasulu nikeshimike kama Mbunge.

"Mimi sio kwamba simuhitaji Mweenyekiti sina shida na mwenyekiti wala kurudi kwenye Baraza la mji wa kasulu mimi nitabaki Kakonko lakini ninacho hitaji niheshima mimi kama mwenyekiti wa UWT na Mbunge wa Mkoa mzima,Siwezi kuleta malalamiko yangu kwamba mtu kanifanyia vurugu nyumbani kwangu nisisikilizwe na hata Zinduse mwenyewe amekwisha lizika na Mwenyekiti",alisema Ngezabuke.

No comments:

Post a Comment