December 19, 2016

KAMPUNI JUNACO YAZINDUA KIFAA CHA KISASA CHA KUZIMA MOTO DAR.

1
George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus akionyesha moja ya kifaa cha kuzima moto kinachoweza kufungwa katika mitambo mbalimbali chenye uwezo wa kuzima moto katika hatua za awali kabisa kabla ya kuwa mkubwa wakati alipokuwa akielezea ubora wa vifaa hivyo katika kupambana na majanga ya moto kwenye uzinduzi ulifanyika Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam mwishono mwa wiki.
2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimsikiliza George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa akitoa maelezo ya jinsi vifaa hivyo vinavyoweza kuzima moto katika mitambo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam, wa pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies na wa tatu ni Fikili S. Salla Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya moto Jeshi la Zimamoto.
3
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimsikiliza George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa akitoa maelezo ya jinsi vifaa hivyo vinavyoweza kuzima moto katika mitambo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam, wa pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimsikiliza George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa akitoa maelezo ya jinsi vifaa hivyo vinavyoweza kuzima moto katika mitambo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam , wa pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group
5
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimpongeza George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus mara baada ya kumaliza kutoa maelezo yake mbele ya wageni waalikwa wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam, katikati ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies
6
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Biashara wa Kampuni ya JUNACO Group Of Companies Limited Bw. Anic Kashashaakizungimza katika uzinduzi huo.
7
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kifaa hicho cha Firepro mwishoni mwa wiki.
8
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya , Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies na George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo
9
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya , Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies na George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo
****************
Kampuni ya JUNACO Group of Companies mwishoni mwa wiki ilizindua kifaa cha kisasa kinachotumika kuzima moto kwenye makazi ya watu na mitambo kinachofahamika kama ‘FirePro’ ikiwa ni uvumbuzi unaolenga kukabiliana na janga hilo hatari.

Akizungumza wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa kifaa hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuhuduriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambao ya Ndani Balozi Hassani Simba Yahya, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya nchini hapa nchini , Bw Justine Lambert alisema matumizi ya kifaa hicho miongoni mwa watanzania yatasaidia kutaondoa athari za uharibifu wa mali na vifo vitokanavyo na majanga ya moto kwenye makazi ya watu.

“Uvumbuzi na ujio wa kifaa hiki ni ishara kwamba athari zitokazo na majanga ya moto ambayo yamekuwa yakiripotiwa kupoteza maisha ya watanzania na kusababisha umasikini kutoka na uharibifu wa mali sasa linakwenda kwisha,’’ alisema Bw Lambert huku akiongeza kuwa wao kama sekta binafsi wana wajibu wa kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi wake.

Alisema mbali na suala la kuhakikisha usalama wa watanzania, uwepo wa kifaa hicho pia utaongeza ajira kwa wadau wote watakaohusika kwa namna moja au nyingine katika mauzo ya kifaa hicho hapa nchini.

“ Ndani ya miaka minne ijayo Junaco Group of Companies tunarajia kutengeneza ajira zipatazo 780 zitakazohusisha wauzaji, wasambazaji na wataalamu wa kufunga kifaa hiki kote nchini,’’ alisema.

Kwa upande wake balozi Simba ambae alimuwakilisha waziri wa wizara hiyo Bw Mwigulu Nchemba alisema serikali imekuwa ikiridhishwa sana hasa pale inapopokea taarifa za uwepo wa teknolojia mpya zinazolenga kutatua changamoto zinazowakibili wananchi wake kuisalama kama hiyo ya uzinduzi wa kifaa cha ‘FirePro’ huku akitoa wito kwa kampuni hiyo kutumia fursa za kiuwekezaji kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vifaa kama hivyo hapa nchini.

“Ujio wa kifaa hiki hapa nchini ni wazi kuwa utakuwa na matokeo chanya kijamii na kiuchumi kwasababu mbali na kulinda usalama wa wananchi na mali zao lakini pia utazalisha ajira zaidi ya 800... hongereni sana naimani mtafikiria pia kuanzisha kiwanda kitakachowezesha uzalishaji wa vifaa hivi hapa nchini,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Meneja Maendeleo wa Mradi huo Bw, George Michael, teknolijia iliyotumika kutengeza kifaa hicho ni bora zaidi kwa nchi zinazoendelea na ni rafiki pia kwa mazingira.

No comments:

Post a Comment