Na Bety Alex,Arusha
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto Ramadhani Idi
mwanafunzi wa darasa la sita kutoka katika Shule ya Msingi ya Albeije Francosea, amemuomba Raisi John Pombe Magufuli kumsaidia apate
mikono ya bandia ili aweze kutimiza ndoto zake za masomo.
Aidha mtoto huyo ambaye ni mlemavu wa mikono amedai kuwa ili kufanikisha zoezi hilo kunaitajika kiasi cha milioni kumi.
Akiongea juzi kwenye maafali ya sita ya darasa la saba
yaliyofanyika shuleni hapo mwanafunzi huyo alisema kuwa kwa kuwa raisi
magufuli anasisitiza elimu bora ni muimu sana akaweza kumuangalia hata
na yeye.
Ramadhani alisema kuwa kwa sasa anapata shida kubwa sana ya
kuweza kuandika kwani anatumia miguu kwa ajili ya kuandika lakini kama
akipata mikono ya bandia itamsaidia kuandika lakini hata kufanya kazi
nyingine za shule kwa kutumia mikono.
"Mimi namuomba raisi magufuli aweze kuniona katika hali
yangu lakini pia hata wasamaria wema wengine kwani Nina ndoto za kuja
kuwa rubani"aliongeza Ramadhani. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Awali Meneja wa shule hiyo bi Hindu Ally alisema kuwa
mwanafunzi huyo anahitaji msaada mkubwa na jamii inatakiwa iweze
kumsaidia kwa kuwa mpaka sasa ameonesha moyo wa masomo.
'Tukiangalia ripoti za mwanafunzi huyu kwa kweli
zinaridhisha sana akifeli sana unakuta kashika nafasi ya tatu na hapo
ana mikono anatumia miguu yake kuandika na ana ndoto za kuwa
rubani"aliongeza Hindu.
Hataivyo kwa upande wa baba mzazi wa mwanafunzi huyo,Idi
Rashidi alisema kuwa wameshafanya mikakati mbalimbali ya kuweza
kumsaidia mwanafunzi huyo lakini wameambiwa na madaktari bingwa kuwa
msaada wa kuweza kupata mikono ya bandia upo nchini Canada.
Idi alisema kutokana na hali ya maisha wameshindwa kutimiza hilo ingawaje mtoto ana moyo wa kupenda na kujali masomo sana.
No comments:
Post a Comment