Father Kidevu Blog , Arusha
MBUNGE Godbless Lema wa Arusha mjini leo ameshindwa kupata dhamana ya kutoka rumande baada ya mawakili wa serikali kutoa pingamizi la rufaa.
Mawakili wa serikali wakiongozwa na Martenus Marandu
waliwaambia waandishi wa habari kuwa waliweka pingamizi kuwa upande wa
mshtakiwa walipaswa kupeleka notisi ya kusudio ya kukata rufaa na sio
kukata rufaa kama walivyofanya.
Akizungumza nje ya Mahakama hiyo wakili wa upande wa
mhishatakiwa Peter Kibatala alisema kesi hiyo itasikilizwa kwa njia ya
majibishano ya barua Novemba 30 ambapo upande wa serikali utatakiwa
kuwasilisha hoja zao majira ya sa mbili asubui, huku upande wa
mhishatakiwa lema ukitakiwa kuwasilisha majibu ya hoja hiyo majira ya
saa sita mchana na upande wa serikali watapaswa kujibu hoja ya upande wa
mshitakiwa majira ya saa tisa alasiri.
Mahakama hiyo inatarajia kutoa uamuzi juu ya pingamizi
hilo Desemba 2, majira ya saa tatu asubuhi huku mshitakiwa
akirudishwa rumande hadi tarehe hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Mahakamani hapo mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, Amani Golugwa
kimelaaani hatua hiyo na kuitaka Mahakama itende haki juu ya shauri la Mbunge huyo kwani wanashindwa kuelewa ni kitu gani kinachofichwa katika
mwenendo wa shauri hilo.
No comments:
Post a Comment