October 10, 2016

YALIYOJIRI TBL MBEYA WALIPO SHEREHEKEA MAFANIKIO YA KIWANDA

 Baadhi ya wafanyakazi wakisheherekea mafanikio ya kiwanda mitaani
 Baadhi ya wafanyakazi wakisheherekea mafanikio ya kiwanda mitaani
 Mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu akipokea cheti cha pongezi
 
Mazoezi ya viungo nayo yalifanyika.
Hivi karibuni kwa mara nyingine kiwanda cha TBL cha Mbeya kilitangazwa kuwa kiwanda bora cha kutengeneza bia barani Afrika na kunukiwa tuzo katika hafla ya SABMiller iliyofanyika nchini Afrika Kusini.

Wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki waliitumia siku nzima kusheherekea mafanikio hayo makubwa ambayo yaliambatana na kufanya mazoezi chini ya Mpango wa kampuni wa Afya Kwanza,kuandamana mitaani kuonyesha tuzo waliyopata kwa wananchi,kutunuku vyeti kwa wafanyakazi wa muda mrefu pia kulikuwepo na hafla kubwa ya kupongezana iliyohudhuriwa na wafanyakazi na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment