Wahitimu katima Shule ya Sekondari ya Abbey Abasia wakionesha mambo mbalimbali waliyojifunza katika masomo ya Sayansi.
Wahitimu wa kudato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Abbey Abasia wakiwa katika maandamano kabla ya kuanza mahafali yao.
Mkuu wa shule ya sekondari ya Abbey Abasia ya Ndanda, Faza Augustine Ombay akimwonyesha mbunge wa jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe mradi wa maji taka unaojengwa shuleni hapo.
Mbunge wa jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe akipokea sehemu ya zawadi ya madawati 50 aliyopewa na uongozi wa shule ya Sekondari ya wavulana ya Abbey iliyopo Masasi wakati wa mahafali ya saba ya kidato cha Nne.Kulia ni Msaidizi wa Abate Abasia ya Ndanda na paroko wa Parokia ya Ndanda,Faza Silvanus Kessy, akifuatiwa na mkuu wa shule,Faza Augustine Ombay.Aliyesimama kushoto ni Diwani wa kata ya Mwena, Nestory Chilumba.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Abbey iliyopo Ndanda wilayani Masasi wamewataka wazazi kuwaacha watoto wao kujichagulia masomo wanayotaka ili kutimiza ndoto zao badala ya kuwawekea msukumo katika masomo ya Sayansi pekee na kuyaacha masomo ya biashara na sanaa.
Pia, jamii imetakiwa kutambua jukumu la kuwalea watoto ili kuwa na nidhamu ni la wazazi na walezi badala ya kuwaachia walimu pekee kwa manufaa ya kuwa na Taifa bora.
Hata hivyo wazazi wameaswa kipindi watoto wao wanapokuwa likizo wasiwapeleke kwenye masomo ya ziada maarufu tuition na badala yake wawapatie kazi za nyumbani kwani wanachanganywa na masomo ya ziada.
Wito huo umetolewa na msaidizi wa Abate Abasia ya Ndanda na paroko wa parokia ya Ndanda,Faza Silvanus Kessy wakati wa mahafali ya saba ya kidato cha nne shuleni hapo na kuwataka wazazi na walezi wote wanaowasomesha watoto wao shuleni hapo kuacha kuwapeleka katika masomo ya ziada.
“Nidhamu ya ndio matokeo mazuri kama atakuwa na ushirikiano na mshikamano hawezi kufanya vibaya kwasababu kila atakachoambiwa lazima atafuata ,hivyo ni ,ni jukumu la wazazi pia katika kulea watoto , niwaonye sana na kitu kinachoitwa tuition (masomo ya ziada) kama una mtoto wako anayesoma hapa ni marufuku kumpeleka tuition na masomo ya ziada ya mitaani huko wannachakachuliwa motto anashindwa kujua kipi ni kipi,wakirudi likizo wapeni kazi za kupika, kufua, kuosha vyombo na bustani,"alisema faza Kessy
Kwa upande wake mkuu wa shule,Faza Augustine Ombay aliitaka seerikali kuacha kuingiza siasa katika masomo kwani wanaharibu mfumo na hivyo kuwelka taifa katika hatari .
"Nimpongeze sana rais katika suala la madawati amefaulu,lakini mbunge wa jimbo la Ndanda uko hapa niwaombe sana nyie ndio wenye bunge tunaiomba serikali isilete siasa katika elimu mtaangamiza kizazi cha sasa na kijacho,mkiweka siasa mtaharibu mfumo na hata kwa Mungu mtahukumiwa na badala yake waangalie ni kwa namna gani wataboresha miundombinu mingine "alisema Ombay
Matokeo ya mwaka jana ilikuwa na wahitimu 111 ambapo wanafunzi 95 walipata ufaulu wa daraja la kwanza, wanafunzi 14 daraja la pili na wawili daraja la tatu.
Hata hivyo, mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa jimbo la Ndanda Cecil Mwambe, aliwataka wazazi kuwaandalia watoto wao mazingira mazuri ya elimu ya chini ili waweze kupata nafasi ya kusoma katika shule hiyo na kuondokana na malalamiko.
"Jamani tuachanae na kulalamika kuhusu watoto wetu kupata elimu inayotakiwa, ifahamike maandalizi yanayofanyika shuleni hapa ni mazuri, elimu bora ni mchakato sisi tulio wengi hatujajiandaa ndio sababu zinazopelekea wahitimu wa ukanda huu kuwa wachache,vigezo vya kuingia Abbey sio dini wala ukabila bali ni ufaulu na nidhamu kwahiyo ndugu zangu tubadilike, "alisema Mwambe na kuongeza:
"Tusiwe watu wa kulalamika,tusidanganyane kuna elimu bora ni lazima iwe ya gharama,wazazi waunge mkono kupata elimu bora tupate wataalamu wa baadaye ,"alisema Mwambe
Hatika hatua nyingien mbunge huyo alimwaguza diwani wa kata ya Mwena, Nestory Chilumba kushirikiana kwa kushirikiana ma kamati ya uongozi ya shule kuona ni kwa namna gani watamaliza tatizo la upigaji wa mziki jirani na shule hiyo hali inayopelekea baadhi ya wanafunzi kutoroka.
Hata hivyo uongozi wa shule hiyo ulitoa madawati 50kwa mbunge huyo kama zawadi ambapo atayagawa katika baadhi ya shule.
No comments:
Post a Comment