Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Bank ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga akizungumza machache wakati wa kuzindua wiki ya huduma kwa wateja katika Benki ya UBA Tanzania Mapema jana asubuhi. Wiki hii ni wiki ya huduma kwa wateja duniani ambapo Bank ya UBA Tanzania imedhamiria kutoa wafanyakazi shupavu ambao watawahudumia vyema wateja wao na kufurahia huduma za benki hiyo inayofanya vizuri
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Bank ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga akizungumza na wafanyakazi pamoja na wateja wa Benki ya UBA Tanzania wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja
Wateja wa Bank ya UBA Tanzania pamoja na wafanyakazi wa bank hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya wiki ya huduma kwa wateja kuzinduliwa
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Bank ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga akimpa zawadi ya fulana mmoja wa wateja waliofika katika benki hiyo wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja mapema leo
Mteja wa UBA Tanzania akipokea zawadi kutoka Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Bank ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga
Baadhi ya wafanyakazi na wateja wa bank ya UBA Tanzania wakikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja ambapo wiki hii bank ya UBA Tanzania imedhamiria kuhakikisha wafanyakazi wake wanatoa huduma bora zaidi na kumfanya mteja kufurahia zaidi na zaidi kuliko siku za kawaida
baadhi ya wafanyakazi wa UBA Bank
Baadhi ya wateja wakipata huduma za kifedha ndani ya bank ya UBA Tanzania mara baada ya kuwasili kwenye bank hiyo wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
No comments:
Post a Comment