Waziri waViwanda,Biashara na
Uwekezaji,Mh.Charles Mwijage (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na Wafanyakazi wa TBL Group wakati wa hafla ya kutangaza chapa bora 50
za kitanzania katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City
mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (kulia) na Maofisa wengine wa kampuni
wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kutangaza na kukabidhi tuzo kwa
chapa bora za kitanzania liyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mwishoni mwa
wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin
(kushoto) akingalia tuzo za chapa ambazo kampuni yake imejishindia (kulia) ni
Meneja wa Chapa ya Konyagi,Martha Bangu,(katikati) ni Meneja wa Chapa ya bia ya
Kilimanjaro,Pamela Kikuli.
Wafanyakazi wa TBL Group wakionyesha vyeti vya
tuzo ambavyo kampuni imeshinda katika shindano la Chapa bora 50 za kitanzania.
Mameneja wa chapa za TBL Group zilizoshinda
wakiwa na wawakilishi wa makampuni mengine.
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samiha Hassan Suluhu
akimpongeza Aisa wa TBL Group,Edith Bebwa
Meneja wa Chapa ya Bia ya Kilimanjaro ,Pamela
Kikuli,akipokea tuzo ya chapa hiyo kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Waziri wa
Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage.Wengine pichani ni wajumbe wa
kamati ya maandalizi ya hafla hiyo.
Meneja wa Chapa ya Konyagi ,Martha Bangu
,akipokea tuzo ya chapa hiyo kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Waziri wa
Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage.Wengine pichani ni wajumbe wa
kamati ya maandalizi ya hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakifuatilia
matukio wakati wa hafla hiyo.
Chapa cha vinywaji vya Bia ya
Kilimanjaro,Konyagi na Dodoma Wine zinazozalishwa na viwanda vya TBL Group,
mwishoni zimetangazwa kuwa chapa bora katika shindano la kuhamasisha watanzania
kutumia bidhaa za Tanzania lililoandaliwa na taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania
(TPSF) kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambapo chapa
50 zimepata tuzo ya ubora.
Hafla ya kutangaza na kutoa tuzo hizo ilifanyika
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambapo mgeni wa heshima alikuwa ni
Makamu wa Rais,Mh.Samia Hassan Suluhu pia ilihudhuriwa na viongozi wa taasisi
za serikali na watendaji wakuu na wafanyakazi wa makampuni mbalimbali binafsi
ambao bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda vyao yalikuwa yameingizwa kwenye
shindano
Akihojiwa na waandishi wa habari muda mfupi
baada ya hafla hiyo,Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema
kuwa kampuni inajivunia kwa chapa zake tatu kuweza kushinda na kuwa
miongoni mwa chapa bora 50 na kutunukiwa tuzo za ubora.
“Tunazipongeza taasisi hizi ambazo zimeandaa
shindano hili la Fahari ya Tanzania kwa kuwa linawezesha wazalishaji wa Tanzania
kujikita kwenye uzalishaji wa bidhaa bora za kuweza kushindana kwenye masoko ya
hapa nchini na kwenye ngazi ya kimataifa “.Alisema Jarrin.
Alisema kuwa pia hatua ya kuzinduliwa kampeni ya
kuwahamasisha watanzania kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ni nzuri kwa
kuwa ikifanikiwa itakuza uchumi wa nchi kwa haraka na kupanua wigo
wa ajira nchini kwa kuwa mahitaji ya bidhaa yanavyozidi kuongeza kwenye
soko ndivyo mapato ya makampuni yanaongezeka na kuiwezesha kuchangia pato kubwa
la serikali kwa njia ya kulipa kodi na kuajiri watu wengi zaidi.
“Hizi ni dalili nzuri katika kipindi hiki
ambacho serikali imetangaza mkakati wa kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya
viwanda.TBL Group tuaendelea kuunga mkono mkakati huu kwa kuwa tayari
tumeishaanza kuutekeleza kwa kuhakikisha uwekezaji wetu unazidi kuleta tija na
kuleta mabadiliko kwa jamii.Viwanda vyetu hivi sasa ni tishio kwa kuzalisha
bidhaa bora mpaka kwenye ngazi ya kimataifa na vinashikilia rekodi ya kufanya
vizuri katika bara la Afrika”.Alisema.
Aliwashukuru wafanyakazi wote wa kampuni hiyo
kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha inazidi kupata mafanikio
siku hadi siku “Mafanikio haya yote tunayoendelea kuyapata yanatokana na
jitihada za kufanya kazi kwa bidii kwa kila mfanyakazi wa kampuni”.Alisema
Roberto.
TBL Group mbali na baadhi ya chapa zake kuingia
katika chapa bora 50 nchini (Top 50 Tanzanian Brands 2016) pia
inashikilia tuzo mbalimbali baadhi zake zikiwa ni Tuzo ya Mzalishaji Bora,Tuzo
ya Mwajiri bora, na Tuzo ya Mlipa Kodi Bora.
No comments:
Post a Comment