Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Devis Deogratius akiongea na mawakala na wageni waalikwa
Mfanyabiashara Julius
Masalu mkazi wa Mwanza (katikati) akipokea funguo za gari alilojishindia katika
droo ya promosheni ya Nunua,Uza ,Shinda na Konyagi iliyohusisha mawakala wa
kuuza bidhaa za kampuni ya Tanzania Distillers Ltd (TDL) kutoka kwa Meneja wa
Chapa ya Konyagi,Martha Bangu (Kulia),anayeshuhudia kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa TDL,Devis Deogratius. Droo ya pili ya promosheni hiyo ilifanyika mwishoni
mwa wiki katika viwanja vya hoteli ya Kili Home mjini Moshi mwishoni mwa wiki
ikihusisha washiriki 31 kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa.
Mfanyabiashara Julius
Masalu mkazi wa Mwanza (katikati) akipokea funguo za gari alilojishindia katika
droo ya promosheni ya Nunua,Uza ,Shinda na Konyagi iliyohusisha mawakala wa
kuuza bidhaa za kampuni ya Tanzania Distillers Ltd (TDL) kutoka kwa Meneja wa
Chapa ya Konyagi,Martha Bangu (Kulia). Droo ya pili ya promosheni hiyo
ilifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya hoteli ya Kili Home mjini
Moshi mwishoni mwa wiki ikihusisha washiriki 31 kutoka mikoa ya kanda ya
kaskazini na kanda ya ziwa.
Mawakala wa Konyagi wakiserebuka
wakati wa hafla hiyo.
Meneja Masoko wa TDL,George Kavishe
akiwashukuru mawakala walioshiriki kwenye promosheni hiyo
MFANYABIASHARA
Julius Masalu (58) mkazi wa Mwanza ameibuka mshidi wa gari aina ya Eicher
lenye thamani ya shilingi milioni 56 katika mzunguko wa pili wa
bahati nasibu ya Promosheni ya Nunua,Uza ,Shinda na Konyagi iliyohusisha
mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya Tanzania Distillers Ltd (TDL).
Droo ya pili ya promosheni
hiyo ilifanyika katika viwanja vya hoteli ya Kili Home mjini Moshi
mwihoni mwa wiki ikihusisha washiriki 31 kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na
kanda ya ziwa na kusimamiwa na afisa wa Bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha
Humudi Abdul Hussein.
Akiongea kwa furaha
baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Masalu alisema ametoka Mwanza akiamini kuwa
atajishindia gari hilo na kwamba bahati nasibu hiyo imeendeshwa kwa uwazi na
hakuna upendeleo unaoweza kufanyika.
“Katika bahati nasibu
hii hakuna longo longo,shindano limeendeshwa kwa uwazi mkubwa sana na
namshukuru Mungu kwa kuweza kupata zawadi hii ya gari itanisaidia sana katika
kusambaza bidhaa za kampuni ya konyagi kwa wateja wangu,” alisema
Masalu.
Kaimu Meneja Mkuu
wa Konyagi, Devis Deogratius alisema dhumuni ya promosheni hiyo ni
kukuza uhusiano wa kibiashara na wasambazaji wa bidhaa za TDL pamoja na
kuwapatia kifaa kitakachosaidia katika kupanua masoko ,kusambaza na kuongeza
ufanisi.
“Safari ilianza mwezi wa
saba hadi mwezi wa tisa ,kumekuwa na usawa katika mchakato huu wa kumpata
mshindi na hakuna upendeleo wowote ,wale ambao wamefikia malengo wamefika
katika promosheni hii na kuwepo hali ya usawa katika kushinda zawadi ya
gari”alisema Deogratius.Alisema mbali na mshindi huyo wa gari katika droo
hii ya kwanza washiriki watano walibahatika kujishindia katoni 10
za Konyagi kila mmoja.
Baadhi ya washiriki
katika droo hiyo, Mkamba Zephania na Joas Muganyizi walisema
wameridhishwa na mchakato mzima ulivyofanyika katika kuchezesha droo na wala
hapakuwa na kasoro ama udanganyifu wowote.
“Kampuni ya TDL kupitia
bidhaa yake ya Konyagi katika promosheni ya Nunua Uza,Shinda na Konyagi
imesaidia kuwakutanisha wafanyabiashara wa maeneo mengine ya kanda ya Kaskazini
na kanda ya ziwa hali inayochangia kuongeza wigo katika kufanya
biashara”.Alisema Muganyizi.
Washindi wengine
waliojinyakulia katoni 10 kila mmoja za bidhaa ya Konyagi na maeneo wanayotoka
kwenye mabano ni pamoja na Linus Mathew (Kagera) Msemo Enterprises (Arusha)
,Joace Muganyizi(Bukoba) Mkamba Zephania (Bariadi) na Yohana Masunga (Geita).
Huu ni mzunguko wa pili wa
droo ya bahati nasibu ya Promosheni ya Nunua Uza,shinda na Konyagi ambapo
katika droo ya kwanza mfanyabiashara Grace Oroki, mkazi wa Jijini Dar es
salaam, alijinyakulia gari kwa mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya TDL wa
mikoa ya Nyanda za juu Kusini na Pwani.
No comments:
Post a Comment