September 09, 2016

WAZIRI NDALICHAKO AKAGUA CHUO KITAKACHOPOKEA WANAFUNZI KUTOKA UDOM WILAYANI KASULU



Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi wakikagua ufanyaji wa mitihani ya Darasa la saba 2016 katika Shule ya Msingi Mwenge, iliyopo Wilayani Kasulu juzi.                        
 Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, (kulia) akizungumza jambo na wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Mwenge ya Wialayani Kasulu wakati alipokagua ufanyaji mitihani hiyo kitaifa. Pamoja nae ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi.                 
 Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi (aliyesimama) akitoa taarifa ya Wilaya hiyo kwa  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako,
 Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi (kushoto) akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kukagua miundombinu ya Chuo cha Elimu ya Taifa Kasulu tayari kwa kupokea wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).


Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi (kushoto) na viongozi wengine wa Chuo cha Elimu Kasulu wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, alipokagua miundombinu ya Chuo cha Elimu ya Taifa Kasulu tayari kwa kupokea wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

No comments:

Post a Comment