September 13, 2016

WAFANYAKAZI TBL GROUP WALIVYOSHIRIKI TAMASHA LA MASHINDANO YA MBUZI

Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (aliyeshika mbuzi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi baada ya mbuzi wao kushinda

 Meneja wa bia ya Kilimanjaro,Pamela Kikuli akikabidhi hundi ya udhamini

 Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kwenye tamasha.

 wafanyakazi wa TBL wakiendelea na yao
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa waandamizi wa kampuni hiyo kwenye tamasha

 Timu ya kikosi cha mbuzi cha Kilimanjaro ndani ya uwanja

 Furaha iliendelea
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya TBL Group,Roberto Jarrin aliungana na wafanyakazi wa kampuni hiyo katika tukio muhimu la kuchangisha fedha za kukabiliana na changamoto za kijamii kupitia mchezo wa mashindano ya mbuzi uliofanyika kwenye viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mwaka huu kampuni imedhamini mashindano haya yaliyolenga kukusanya fedha za kusaidia vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji maalum kupitia bia yake ya Kilimanjaro.

Kama ilivyo moja ya sera ya kampuni inayoelekeza wafanyakazi wake kutenga muda wao kushiriki katika masuala ya kusaidia jamii,wafanyakazi wa TBL Group walijitokeza kwa wingi na walikuwa na furaha  wakati wote ya kushiriki tukio hili muhimu linalolenga kuleta mabadiliko kwenye jamii.

No comments:

Post a Comment