September 18, 2016

WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE MBEYA WATEMBELEA KIWANDA BORA CHA BIA AFRIKA

Fundi Sanifu wa maabara ya kiwanda cha Bia cha TBL-Mbeya, Phili Said (kulia) akitoa maelekezo namna pombe inavyopimwa katika maabara yao kwa waandishi wa habari wanawake wa Mkoa wa Mbeya.
 Meneja wa kiwanda cha TBL Mbeya,Jemedari Waziri ,akiongea na waandishi wa habari wanawake
 Waandishi wa habari wakiangalia malighafi ya Shahiri inayotumika kutengenezea bia.
 Waandishi wakitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda
Waandishi wakiwa wameshikilia ngao ya ushindi na cheti ambacho kiwanda kimepata hivi karibuni
****************
 chache baada ya kiwanda cha bia cha TBL Mbeya kutangazwa kuwa kiwanda bora barani Afrika,pongezi kwa mafanikio hayo zimekuwa zikitolewa kutoka makundi mbalimbali ya kijamii mkoani humo na kupokea maombi ya kutembelewa kwa ajili ya mafunzo na kujionea jinsi kinavyoendesha shughuli zake.

Moja ya kundi lililoguswa na mafanikio hayo na kutembelea kiwanda hicho ni wanachama kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake mkoani humo ambao baadhi ya wanachama wake wametembelea kiwanda na kupata fursa ya kutembezwa idara mbalimbali kiwandani hapo na kuongea na Meneja wa kiwanda,Mhandisi Jemedari Waziri.

Waziri aliwaelezea waandishi hao kuwa siri ya mafanikio hayo ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni kuanzia kwenye mitambo ya uzalishaji mpaka kwenye wafanyakazi walioajiriwa na kiwanda bila kusahau mifumo ya uendeshaji viwanda ya kisasa iliyowekwa na kampuni.

Alisema kiwanda kitaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine mkoani humo katika miradi mbalimbali ya kubadilisha jamii hususani katika sekta ya utunzaji Mazingira na kulinda vyanzo vya maji.

No comments:

Post a Comment