Mkurugenzi
wa Ufundi wa TBL Group,Givan Van Wijk akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kushoto kwake ni Maofisa Waandamizi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi
wa Ufundi wa TBL Group,Givan Van Wijk akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kushoto kwake ni Maofisa Waandamizi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi
wa Ufundi wa TBL Group,Givan Van Wijk (kulia) katika picha ya pamoja na baadhi
ya Maofisa Waandamizi wa kampuni hiyo.
*****************
MKURUGENZI wa ufundi wa TBL Group na viwanda
vya SABMiller kanda ya Afrika Mashariki,Gavin Van Wijk,amesema mkakati wa
serikali ya tano wa kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda unaweza kutekelezeka
na kuleta maendeleo makubwa kwa nchi.
Alisema
kinachotakiwa kufanyika haraka ni kujifunza kutoka nchi zilizofanikiwa katika sekta ya viwanda na kutumia mifumo ya
uendeshaji viwanda kwa tija na ufanisi
inayotumika katika nchi hizo ambayo imeziwezesha kuwa na viwanda imara.
Akiongea
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam jana,Wijk alisema
kampuni ya TBL Group imeanza kuonyesha njia kuwa Tanzania ya viwanda
inawezekana kutokana na viwanda vyake vya kutengeneza bia vilivopo nchini kuwa
miongoni mwa viwanda bora vinavyoongoza barani Afrika kwenye mtandao wa viwanda
vilivyopo chini ya kampuni ya SABMiller. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
“Kwa miaka
6 mfululizo viwanda vya Tanzania vimekuwa vikishinda tuzo mbalimbali za ubora na
kuwa tishio kwa viwanda vingine vilivyopo kwenye nchi nyinginezo za Afrika na mwaka huu rekodi ya kiwanda bora
barani Afrika inashikiliwa na kiwanda cha TBL Mbeya wakati nafasi ya pili inashikiliwa na kiwanda
cha Mwanza pia viwanda vya Arusha navyo viko kwenye nafasi za juu na bidhaa
zinazotengenezwa na viwanda hivi ni tishio katika masoko ya kimataifa”.Alisema.
Alisema
siri ya mafanikio haya ni kuhakikisha mifumo ya kampuni ya uzalishaji wenye
tija inafuatwa na matokeo yake ni kupatikana kwa uzalishaji
wenye tija na viwango vya kimataifa.”TBL Group tunatekeleza programu ya
uendeshaji viwanda kwa ufanisi ya kampuni ya SABMiller inayojulikana kama
Manufacturing Way ambayo ikitekelezwa ipasavyo popote pale lazima ufanisi
upatikane”.Aliseme Wjik.
Aliongeza
kuwa inafurahisha kuona watanzania wapo makini kujifunza Programu mbalimbali za
kuleta ufanisi na kuzitekeleza kwa umakini mkubwa na kuwa viwanda vya TBL Group ambavyo vinazidi kuwa
tishio kwa ubora barani Afrika na sehemu nyinginezo duniani vinaongozwa na watanzania na wafanyakazi
katika viwanda hivi ni watanzania wenyewe.
Alisema mafanikio mengine kwa viwanda hivi
yanatokana pia na uwekezaji unaofanyika kila mwaka kwenye mitambo na vitendea
kazi vya kisasa ambapo kampuni inatumia zaidi ya dola milioni 14 katika
uwekezaji wa kufunga za kisasa,uwekezaji ambao pia unaenda sambamba na kuwekeza kwa mafunzo ya
wafanyakazi ili waweze kuitumia kuleta ufanisi.”Tumekuwa tukiendesha mafunzo ya
ndani na nje kwa wafanyakazi wetu wote mara kwa mara kwa ajili ya kuwawezesha
kwenda sambamba na mifumo ya kimataifa ya uzalishaji wenye tija kwenye viwanda
vyetu”.Alisisitiza Wijk.
Mafunzo
wanaoyapata wafanyakazi mbali na kuwasaidia kuleta ufanisi katika kazi zao
viwandani alisema pia yanawasaidia wanapokuwa nje ya kazi za ofisi.Alitoa mfano
kuwa wafanyakazi wanafundishwa kufuata ratiba katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku,kuzingatia
muda,usafi wa mazingira, kuzingatia usalama
kwa kwao binafsi na watu wengine,umuhimu
wa kufanya mazoezi na mambo mengineyo mengi.
Pia
alisema kampuni inatekeleza malengo ya
SABMiller ya ustawishaji jamii na kuleta
maendeleo endelevu ambayo yanashabiana na malengo ya Umoja Wa Mataifa na
utekelezaji wake umeonyesha kuleta manufaa katika sehemu zote ambako viwanda
vya kampuni vilipo.
Baadhi ya
malengo aliyataja kuwa yamelenga kutunza mazingira na vyanzo vya maji,kuwezesha
wazalishaji wanaouzia kampuni malighafi,kuongeza fursa za ajira za moja kwa
moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja “Kampuni imepata mafanikio kwa kuwezesha
wakulima wanaouzia malighafi kupitia mpango unaojulikana kama Go Farming ambao
unaendelea kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.Tumeanza na wakulima wa
Shahiri na Zabibu na tutahakikisha
mpango huu unawafikia wakulima wengi zaidi nchini”.Alisisitiza.
Kuhusiana
na suala la Usalama alisema kuwa limekuwa likipewa kipaumbele katika viwanda
vyake vyote na kutokana na wafanyakazi kupatiwa mafunzo ya usalama mara kwa
mara matukio ya ajali yamepungua kwa kiasi kikubwa ni nadra kutokea pia usalama
hauishii kwa wafanyakazi pekee bali hata kwa wakandarasi wanaofanya kazi
viwandani na kwa wageni wanaotembea viwanda.“Kwenye suala la usalama tumekuwa
tukishinda tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya Usalama mahali pa kazi ya OSHA na
tuzo ya usalama wa viwandani ya kimataifa ijulikanayo kama NOSA kwa kiwango cha
Nyota 5 .
Motisha kwa wafanyakazi alisema ni moja ya
suala ambalo kampuni imekuwa ikilipa umuhimu mkubwa “Motisha hizi zimetuwezesha kupata mafanikio
makubwa na zimepelekea kampuni kushinda tuzo ya Mwajiri bora inayotolewa na
Chama Cha Waajiri Nchini (ATE) na tuzo ya mzalishaji bora inayotolewa na
Shirikisho la Viwanda Tanzania”.
Alimalizia
kwa kusema kuwa kampuni itaendelea kubuni mikakati ya kuendelea kufanya vizuri
katika uzalishaji na kwenye masoko na
kuhakikisha uwekezaji wake unaleta manufaa kwa taifa kuanzia kwenye kuchangia
pato la serikali kwa njia ya kulipa kodi na kuleta mabadiliko kwenye jamii pia kufungua milango kwa viwanda na taasisi
nyingine zinazotaka kujifunza mifumo ya uendeshaji viwanda kwa kufuata mifumo
yenye kuleta tija na ufanisi.
No comments:
Post a Comment