September 29, 2016

MMILIKI WA GHOROFA KARIAKOO AKAMATWA NA MAJI YA WIZI .

Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), limeendelea kufanya opresheni maalum ya kubaini wizi wa Maji kwenye maeneo ya jiji la Dar es salaam na kubaini baadhi ya majengo ya kata ya kariakoo yakiwa yamejiunganishia kinyume cha utaratibu.

Akizungumza katika operesheni hiyo maalum, kiongozi wa operesheni kutoka ofisi ya Dawasco mkoa wa Ilala Bw. Gadimula Temba amesema kuwa wamebaini wizi wa Maji kwenye jengo linalomilikiwa na ndugu Mahsen Mohamed ambapo alikuwa amefungiwa laini ya Majisafi na amekuwa akidai hapati maji kila ifikapo kipindi cha kusoma mita licha ya mita yake kusoma nakuonyesha kuwa ana deni la shilingi laki tisa na ndipo walipokwenda mafundi kuchunguza nakubaini kuwa amejiunganishia laini tatu za majisafi pamoja nakufunga mota yakuvuta maji kwenye laini hizo zisizokuwa na mita.

“leo tumebaini wizi wa Maji kwenye jengo la ndugu Mahsen Mohamed ambaye amekuwa akidai kuwa hapati Maji ya Dawasco kwa muda mrefu licha ya mita yake kusoma nakuonyesha anadaiwa kiasi cha shilingi laki tisa ndipo tukaamua kufanya uchunguzi nakubaini anatumia Maji yetu na pia amejiunganishia laini tatu za maji zisizokuwa na mita pamoja nakufunga mota yakuvuta maji" BOFYA HAPA.


“Ila pia tumebainf2fi kuwa amejiunganisha kwenye huduma ya mfumo wa Majitaka  kinyume cha utaratibu bila kibali kutoka Dawasco na amekuwa akikataa kuwa hatumi mfumo wetu” alisema Temba.

Hata hivyo Dawasco imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kung’oa mota ya kuvuta majisafi, kufunga laini zote za majisafi na ya majitaka pamoja na kumtaka mmiliki wa jengo hilo kufika kwenye ofisi za Dawasco kwa taratibu zingine za kisheria.

Nae afisa mtendaji wa kata ya Kariakoo Bw. Adeltus Kazinduki amewataka wamiliki wa majengo makubwa kariakoo kuachana na tabia ya wizi wa maji kwani ofisi yake kata inashirikiana na Dawasco mkoa wa Ilala kubaini watu wote na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika.

“kwa kweli ofisi yangu ya kata ya kariakoo haitamvumilia mmliki yoyote ambaye anafanya wizi wa Maji kwasababu sisi na Dawasco tumekaa kikao cha pamoja nakukubaliana kuwa na ushirikiano hivyo mmiliki wa jengo lolote atakaye kamatwa atachukuliwa hatua kali za kisheria” alisema Kazinduki.

Hata hivyo mmiliki wa jengo hilo Bw. Mahsen Mohammed hakuweza kupatikana na hata wapangaji wa jengo hilo walidai hawajui makazi yake kwani ni mtu wa kusafiri mara kwa mara .

No comments:

Post a Comment