September 03, 2016

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA APONGEZA SEMINA YA FURSA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Zainab Rajab Telack, akitoa pongeza zake kwa waandaaji wa Semina ya Fursa na tamasha la Fiesta 2016 ndani ya Ukumbi wa Shycom mjini Shinyanga mapema leo.
Msanii wa Bongo Fleva Madee akizungmza jambo kwa niaba ya wasanii wenzake kwenye semina ya Kamata Fursa.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Croup, Ruge Mtahaba, akitoa semina kwa baadhi ya wakazi wa Shinyanga waliojitokeza kwenye semina hiyo.
Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la Fiesta usiku wa leo wakiwa ndani ya Ukumbi wa Shycom ambapo semina ya Kamata Fursa ilikuwa ikifanyikia.
Mkurugenzi wa chuo cha Mlimani Professional Hassani Ngoma akiwapa mbinu za mafanikio wakazi wa Shinyanga kwenye semina ya Fursa.
 Wasanii wakiwa kwenye pozi la pamoja.
Baadhi ya watu waliohudhulia kwenye Semina ya  Fursa. 
**************
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga MH. Zainab Rajab Telack, mapema leo ameipongeza semina ya Kamata Fursa inayoendeshwa sambamba na tamasha la Fiesta 2016, katika Ukumbi wa Shycom uliyopo Shinyanga.

Akizungumza mbele ya wakazi wa mkoa huo waliokuwa wamekusanyika kwa wingi ndani ya Ukumbi huo kwaajili ya kujifunza mbinu mbalimbali za kujikwamua kimaisha, Mh. Zainab alisema kuwa amefarijika na semina hiyo kwani ina lengo zuri la kuwaonyesha fursa mbalimbali wakazi wake.

Aidha  Mh. Zainab amesema kwamba uwepo wa Fiesta umeongeza mapato makubwa mkoani hapo kwani shughuli nyingi za kijamii zimechangamka.

Niwapongeze sana watu wote mliotumia muda wenu kuja kusikiliza mambo mbalimbali kwenye semina hii, naamini kabisa uwepo wenu hapa kila mmoja atavuna jambo la msingi la kuufanya Mkoa wa Shinga uendelee kupanuka kimapato, alisema Mheshimiwa Zaina Rajab.
Mbali na kuipongeza Fursa hiyo Mh. Zainab aliongozana na wasani wote watakao fanya shoo usiku wa leo katika Uwanja wa nje wa Kambalage kwenda kuona maporomoko ya maji ya moto yaliyopo eneo la Uzogole nje kidogo ya mji huo.

No comments:

Post a Comment