September 22, 2016

DC HANDENI.MH GONDWE AFANIKIWA KUTATUA MGOGORO WA MPAKA ULIOKUWA UKIVIHUSISHA VIJIJI VIWILI WILAYANI HANDENI


 Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Gdwin GOndwe akisalimiana na mkazi wa kijiji cha nyasa.

 Mkuu waa Wilaya ya Handeni,Mh Godwin Gondwe  Jana alifanikiwa kusuluhisha mgogoro wa mpaka uliokuwa ukivihusisha vijiji viwili vya kata ya kang'ata wilayani Handeni .Vijiji hivyo ni Madebe na Nyasa ambao walikua hawafahamu mpaka wao unaishia wapi,suluhu hiyo ilifanikiwa kumalizwa na mkuu wa wilaya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Handeni ,Bwa.William Makufwe.

DC Gondwe pia aliwataka wananchi na viongozi wajikite katika shughuli za kimaendeleo badala ya kujikita kwenye suala la mipaka ,Kwa madai  wapate maeneo ya kulima wakati wakigombania maeneo ili wauze. Amewaonya wasiuze ardhi kiholela  na kufanya vizazi vijavyo kuwa watumwa kwenye ardhi yao.
 Mkuu wa wilaya Mh.Godwin Gondwe akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Handeni,Ndugu William Makufwe (pichani kushoto) akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa vijiji vya nyasa na madebe.
 Mwenyekiti wa kijiji cha nyasa  na madebe wakipeana pongezi baada ya kujua mipaka yao huku wakisistizwa kujikita zaidi katika masuala ya maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Gondwe akipeana mkono wa pongezi na Mwenyekiti wa kijiji cha Nyasa baada ya kupata mpaka wa maeneo yao.
Mkuu wa wilaya ya handeni Mh.Gondwe akizungumza na wananchi wa vijiji vya nyasa na madebe akiwakataza wasiuze ardhi kiholela na wasigombanie maeneo ili wayauze.

No comments:

Post a Comment