September 05, 2016

BENKI YA MAENDELEO YADHAMINI SHINDANO LA GOSPEL STAR SEARCH JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Benki ya Maendeleo, Peter Tarimo akisaini mkataba wa udhamini wa shindano la Gospel Star Search (katikati) huku meneja wa Mrado huo wa GSS, Samwel Sasali (kushoto) akishudia tukio hilo lililofanyika leo hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam.
 
 Siku Ya Leo Kamati Ya Gospel Star Search na Kampuni  za Maendeleo Bank na Grace Product Wametiliana saini Mkataba wa Udhamini wa Gospel Star Search 2016. 
 
 Meza kuu.
  Ndugu waandishi wa habari tunashukuru sana kwa kuitikia wito wetu siu ya leo, katika project hii kubwa inayoendelea ya Gospel star search.  BOFYA HAPA KWA TAARIFA ZAIDI

 *************
Tulikwisha kuanza toka na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa mpaka sasa lakini lengo kuu hasa la uwepo wetu hapa siku ya leo ni kuwajuza juu ya uwepo na kutiliana saini na wadhamini wetu ambao wameona ni vyema na tumekubaliana kufanya kazi pamoja katika project hii ya Gospel star search. Nitamkaribisha mwenzangu yeye atasema zaidi kuhusu GSS na hatua tuliofikia mpaka sasa na kuwatambulisha wadhamini wetu. 

LENGO KUU Ahsanteni sana waandishi wa habari kwa kuitikia wito wetu, kama alivyosema mwenzangu lengo letu siku ya leo ni kuwatambulisha wadhamini wetu kwenu na kwa watanzania ,lakini kabla ya kwenda mbali ni vyematukatoa mrejesho mfupi juu ya GSS ilipoanza mpaka hatua tuliofikia kwa mwaka huu. 

GSS ina lengo kubwa ya kutafuta waimbaji wa muzii wa injili na kuwasaidia kujitambua kuwapa nafasi ili kukuza vipaji vyao na kuvifanya vionejkane kwa watu kwaajili ya kua faida kw watu lakini hata kwao wenyewe pia.

Tunaamini sana kipaji kama kikitumika kwa namna ilio sawa kinaweza kubadili kabisa maisha ya mtu na akawa mtu mwingine mwenye maisha bora yalioletwa na kipaji au talanta alionayo hii ndio sababu tumeipa kauli mbiu ya KIPAJI CHAKO… HATMA YAKO. 

Tumeanza na wilaya tatu za mkoa wa Dar es salam kwa sasa, Kinondoni, Temeke pamoja na Ilala na kila sehemu tumechua washiriki wa tano hivyo kua na jumla ya wshiriki 15 kwa wilaya zote 3 ambao hawa ndio wamefanikiwa kuingia hatua ya nuusu fainali. Mchakato wetu umekua na round mbili (2) za mchujo ambazo kwazo ndizo zimetupa washiriki hawa 15 waliopo mpaka hivi sasa. 
Ndugu waandishi wa habari tunashukuru sana wadhamini wetu ambao waliona ni vyeama kushiriki na sisi kwa kutufanyia udhamini kwenye project hii kubwa ya GSS, ambao leo tuko nao hapa kwaajili ya kuwatambulisha rasmi kwenu..ambao ni

 • Maendeleo Bank 
 • Grace Product 
 • Brand exponetial
 • Kiango media 
• Clouds Media Group 
• Fm studios (Faith music lab) 
 • 3D 

Kwa hiyo uwepo wetu hapa ni kuwatambulisha rasmi watu hawa amabao wameona ni vyema kusimama na sisi na pia kutiliana saini mbele yenu kama ishara ya kuingia ubia katika project GSS. Kwa kusema haya sasa nitatoa nafasi kwa wadhamini kusema kdogo ju yao lakini pia juu ya GSS karibuni sana!

 HITIMISHO Pia tungependa kuchukua fulsa hii kutoa wito na hamasa kwa makampuni mengine ambao wanaweza kushirikiana na sisi kama wadhamini kweye project hii ya GSS bado milango ipo wazi na tutafurahi sana kushirikiana na ninyi katika project GSS 2016 ,Uwanja wetu ni mpana na jukwaa letu ni kubwa hivyo itakua ni nafasi ya manufaa kwetu na kwenu pia kama mtaamua kutuunga mkono nkwa udhamibni katika project hii ya GSS 2016 kwa hatua zilizosalia za nusu fainali na fainali. Baada ya kusema haya ninaomba niwashukuru tena kwa uwepo wenu na hayo ndio yalikua maelezo juu ya lile lililotuweka hapa siku ya leo.

No comments:

Post a Comment