Waziri Nape akizungumza kabla ya kukabidhiwa uwanja huo Agosti 22, 2016. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Elisante Ole Gabriel, na kushoto ni mshauri wa ujenzi, Injinia Aloyce Peter Mush.
WaziriNape, (wapili kushoto), Katibu Mkuu Profesa Ole Gabriel, (wakwanza kushoto),Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo, Alex Makoye
Nkenyenge, (watatu kushoto) na Injinia Mushi, wakikagua uwanja huo
Waziri Nape, akikagua nyasi bandia uwanjani
Alama ya uwanja wa Uhuru ni jukwaa hili kuu, kama linavyoonekana leo Agosti 22, 2016. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Vyoo vya kisasa, (kushoto) wanawakena kulia wanaume
Waziri akimpongeza Meneja wa Kampuni ya Kichina ya Beijing Construction Engineering Group Company Limited, (BCEG),
Cheng Long Hai
Cheng Long Hai
Katibu Mkuu Profesa Ole Gabriel, (kulia) na Meneja Mkuu wa (BCEG),
Cheng Long Hai, wakisaini hati za makabidhiano ya uwanja mbele ya Waziri Nape
Waziri Nape akishuhudia makabidhiano ya hati kuthibitisha sasa uwanja uko mikononimwa serikali
Profesa Gabriel
Injinia Mushi
Cheng Long Hai
Waziri akizungumza jambo wakati wa ukaguzi wa nje wa uwanja huo.
*************
*************
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
SERIKALI
imekabidhiwa rasmi uwanja wa Taifa wa Uhuru, (pichani juu), jijini Dar es Salaam, leo Agosti
22, 2016, baada ya ukarabati mkubwa wa uwanja huo kukamilika.
Akipokea uwanja huo kwa niaba ya
Serikali, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amewapongeza
wakandarasi ambao ni kampuni ya China ya Beijing Construction Engineering Group Company Limited, (BCEG), na
mshauri mwelekezi wa uwanja huo kampuni ya kizalendo chini ya uongozi wa ke,
Injinia Aloyce Peter Mushi kwa kazi nzuri iliyofanyika licha ya mikwamo ya hapa
na pale.
“Ndugu
zetu Wachina, wameonyesha sio tu uhusiano mzuri bali wameonyesha kuwa wao ni
ndugu zetu, kwani walishiriki wakati nchi yetu ikipata uhuru laini toka wakati
huo hadi hivi sasa, bado wanashiriki katika kusaidia kuimarisha uchumi wetu,”
alisema.
Waziri
Nanuye aliwataka watumiaji wa uwanja huo kulipa ada za matumizi kama
inavyostahili, ili hatimaye fedha hizo ziweze kugharimia matunzo ya uwanja.
Akitoa
taarifa ya ujezni huo, mshauri huyo mwelekezi wa ujenzi, Injinia Aloyce Peter
Mushi alisema, uwanja huo una uwezo wa kuchukua watu milioni 22 na ulikamilika
na kuanza kutumika kwa mara ya kwanza Mei 22, 2015.
Naye
Meneja Mkuu wa Kampuni ya BCAG, Cheng Long Hai, alisema, uwanja huo umewekewa
mifumo yote muhimu kama vile tangi la kuhifadhia maji na mifumo ya maji taka,
na kuishukuru serikaliya Tanzania kwa kuiaminikampuni yake kutekeleza mradi huo
mkubwa.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante
Ole Gabriel, alisema, amekuwa akipokea maombi mbalimbali ya wanamichezo na watu
wengine kuomba kuutumia uwanja huo na kuwahakikishia kuwa utaratibu unapangwa
ili watanzania waanze kufaidi matunda ya uwanja huo ambao kutokana na ukongwe
wake ulipachikwa jina la shamba la bibi.
“Nitoe
rai tu kwa watanzania, leohii Agosti 22, 2016 ambapo tumekabidhiwa uwanja huu
rasmi ukiwa umekamilika, naomba hilo jina la shambala bibi nalo lifikie kikomo
kwani uwanja huu sa sa unauonekano mpya na wa kisasa.” Alisema Profesa Gabriel.
Ukarabati
huo mkubwa ulihusisha ujenzi wa jukwaa na paa, ikiwa ni pamoja na miundombinu
mingine ya uwanja kama vile, mifumo ya kusambaza maji, na kutoa maji taka,
uwekani wa tanki la kuhifadhia maji, pamoja na ujenzi wa vyoo vya kutosha
uwanjani.
No comments:
Post a Comment