August 31, 2016

WAUZAJI BIDHAA ZA TBL GROUP KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

 Wafanyabiashara wa rejareja wanaouza bidhaa zinazozalishwa na viwanda tanzu vya TBL Group wa mkoani Iringa wakifuatilia mafunzo ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na  taasisi ya TAPBDS kwa udhamini wa TBL Group kupitia mpango wake wa Retail Development Programme.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ujasiriamali wakitunukiwa vyeti vya ushiriki kutoka Meneja Mauzo wa TBL kanda ya Iringa-Raymond degera
****************
Wafanyabiashara wadogo wanaouza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya kampuni ya TBL Group  nchi nzima watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali yaliondaliwa na kampuni kupitia mpango wa kuendeleza wajasiriamali wadogo inaoshirikiana nao kibiashara ujulikanao kama Retail Development Programme (RDP).

 Mafunzo haya katika awamu hii yatawafikia zaidi ya wafanyabiashara  1,838 kutoka kanda mbalimbali za mauzo za kampuni nchi nzima katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia sasa ukiwa  ni mwendelezo wa mkakati wa kampuni wa kuwawezesha wabia wake inaoshirikiana nao kibiashara kwa kufikisha bidhaa inazozalisha kwa walaji wa mwisho ili waendeshe biashara zao kwa weredi na kupata mafanikio katika biashara zao.

Mtazamo na moja ya  malengo ya kampuni mama ya SABMiller ni ‘Dunia Yenye Nuru Njema’lengo ambalo limelenga kuharakisha ukuaji wa maendeleo ya kijamii kwa kuhakikisha wabia wake wanaouza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyake hususani wafanyabiashara wadogo wanawezeshwa kustawisha biashara zao  ikiwemo kuwawezesha kuishi maisha bora na familia kupitia biashara  zao na kutoa mchango wa kuendeleza jamii wanazoishi na kufanyia biashara zao”.Alisema.

 Mafunzo haya yanaendana na mahitaji ya ujuzi unaopaswa kutolewa kwa wafanyabiashara kulingana na mahitaji yao kutokana na utafiti  uliofanywa na kampuni na kubaini maeneo yenyemapungufu na wameandaliwa mafunzo   yatakayowawezesha kuwa na uelewa mzuri wa kuendesha biashara zao kwa ufasaha.

Mafunzo  yatakayotolewa kwa wafanyabiashara hao  ni kuhusiana na mbinu za kufanikisha mauzo ,nidhamu katika matumizi ya fedha , mahesabu sahihi katika biashara , utunzaji sahihi wa vitabu vya hesabu na mbinu za kukabiliana na ujumla ushindani wa kibiashara ya uuzaji vinywaji  na ujasiriamali kwa ujumla.

 wafanyabiashara  wanapata fursa ya kufundishwa masuala ya usafi na mazingira katika maeneo yao ya biashara  na kanuni nyinginezo za kibiashara ikiwemo taratibu za uendeshaji biashara  kwa kushirikiana  na kampuni ya TBL Group na kutambua bidhaa zinazozalishwa na kampuni  hiyo na kampuni zake tanzu.

Kampuni pia imekuwa ikibuni kampeni mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara wanaouza bidhaa zake lengo kubwa ikiwa ni kuwainua kimaisha na kustawisha biashara zao na kuwajengea uwezo wa kujiamini kibiashara.


No comments:

Post a Comment