Warembo wanaoshiriki
shindano la miss kanda ya kaskazini kutoka katika mikoa ya Arusha,Manyara,Tanga
na Kilimanjaro wakiwa nje ya hotel ya Clous view sehemu ambayo wanafanyia
mazoezi kwa ajili ya shindano hilo linalofanyika july 6 katika viwanja vya
ukumbi wa Triple A FM.
Warembo wanaoshiriki
shindano la miss kanda ya kaskazini kutoka katika mikoa ya Arusha,Manyara,Tanga
na Kilimanjaro wakiwa nje ya hotel ya Clous view sehemu ambayo wanafanyia
mazoezi kwa ajili ya shindano hilo linalofanyika july 6 katika viwanja vya
ukumbi wa Triple A FM.
Na Woinde
Shizza,Arusha
Jamii
imetakiwa kuwapa ushirikiano wa kutosha wasichana wanaoshiriki mashindano
ya urembo kwani mashindano hayo ni kazi kama vile kazi zingine.
Hayo
yamebainishwa na baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la kumsaka
mrembo wa kanda ya Kaskazini (Miss Kanda ya kaskazini 2016)wakati walipokuwa
wakiongea kwa nyakati tofauti na mwanandisi wa habari hizi katika kambi yao
kujiandaa na shindano litakalo fanyika Jumamosi July 6 katika ukumbi wa Triple
A uliopo jijini Arusha
MMoja wa
washiriki hao aliyejitambulisha kwa jina la Mariamu Mohmed (18) Mshiriki kutoka
mkoa wa Manyara alisema kuwa wazazi wengi hususa ni ndugu
wamekuwa wakichukulia shindano hili kama ni sehemu ya uhuni kitu ambacho sio
cha kweli
Alibainisha
kuwa shindano hili ni zuri na linatoa ajira kwa vijana wengi na mbali na ajira
pia linasaidia vijana wengi ambao ni wasichana kujiajiri wenyewe na wengine
kuajiriwa katika sehemu mbalimbali.
Kwa upande
wake mshiriki kutoka mkoani Tanga Rukaiya Hassan (20) alisema kuwa kuingia
katika urembo sio uhuni wala umalaya kwani ,mtu kuwa na tabia chafu kama izi ni
hulka yake mwenyewe na sio mashindano haya ndio yanasababisha mshiriki au
mshindi kuwa muhuni
Aidha mshiriki
kutoka mkoani Arusha Maurine Ayubu (20) alisema kuwa baadhi ya ndugu wa karibu
wamekua wakiwakatisha tamaa washiriki wengine wakiwatenga kutokana na kile
wanachodai kuwa ndugu aliyeshiriki shindano hili ni malaya kitu ambacho sio cha
kweli na kinawakatisha tamaa warembo wengi ambao walikuwa na ndoto ya kushiriki
mashindano hayo.
"unajua
mimi naona kila mtu na tabia yake ambayo anayo lakini swala la kusema kuwa
kushiriki shindano hili ni umalaya sio la kweli nanaomba ndugu a ambao
wananduguzao wanashiriki mashindano ya umiss wawape ushirikiano wa kutosha
kwani hii ni kazi kama kazi zingine"alisema mshiriki kutoka mkoani
Kilimanjaro Navia Samwel.
Aidha pia
aliongeza kuwa kwa upande wake anaamini kabisa atashinda katika kinyaganyiro
hicho kwani anajiamini na aliwasihi wenzake iwapo itatokea mtuakitolewa nje
asibaatike kuingia katika hatua yatano bora asikate tamaa kwani anaweza pia
kushiriki katika mambo mengine ikiwa ni pamoja na uwana mitindo.
Kwa upande
wake muaandaaji wa shindano hilo mkurugenzi wa mwandago ivestiment Faustine
Mwandago alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yameshakamilika wanasubiri tu
siku ya tukio ifike kwani warembo wamepikwa wakapikia vya kutosha .
No comments:
Post a Comment