Wafanyakazi wakiwa wanaburudika wakisheherekea
kupata tuzo na NOSA ambayo viwanda vya Via vya TBL Dar es Salaam na TBL Mbeya vimeshinda tuzo ya utekelezaji kanuni za Usalama na
Afya mahali pa kazi kutoka shirikisho la kimataifa la kusimamia masuala
ya usalama mahali pa kazi lenye makao makuu nchini Afrika ya Kusini
lijulikanalo kama National Occupational Safety Association (NOSA).
Wafanyakazi wakipongezana kutokana na mafanikio ya
kampuni ya kushinda tuzo ya NOSA
Wafanyakazi wakipongezana kutokana na mafanikio ya
kampuni ya kushinda tuzo ya NOSA
Wakipata
burudani ya muziki kusheherekea mafanikio hayo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
****************
VIWANDA cha kutengeneza vinywaji vya TBL Dar es
Salaam na TBL Mbeya vimepata tuzo ya utekelezaji kanuni za Usalama na
Afya mahali pa kazi kutoka shirikisho la kimataifa la kusimamia masuala
ya usalama mahali pa kazi lenye makao makuu nchini Afrika ya Kusini
lijulikanalo kama National Occupational Safety Association (NOSA).
Tuzo hii ambayo viwanda vya TBL Group vya
Mbeya,Mwanza na Dar es Salaam vimeipata mfululizo imekuwa ikitolewa kutokana na
kukidhi viwango vya kimataifa vya utekelezaji kanuni za afya,usafi na usalama
mahali pa kazi ambapo wataalamu kutoka taasisi ya NOSA wamekuwa wakija nchini
kufanya ukaguzi kwenye viwanda vyake na vimekuwa vikipata alama ya
kufanya vizuri kwenye kiwango cha nyota nne na nyota tano.
Akiongea wakati wa hafla ya kusherehekea
tuzo hiyo mwishoni iliyofanyika katika kiwanda cha Ilala,Meneja wa
kiwanda cha TBL cha Dar es Salaam,Calvin Martin alisema kuwa kampuni inajivunia
kuendelea kufanya vizuri katika suala la Usalama na Afya mahali pa kazi ambapo
mwaka huu imeshinda kwa kiwango cha nyota tano ambacho ni kiwango cha ufanisi
cha hali ya juu
“Tunayo sababu ya kusherehekea kupata tuzo hii
tena katika kipindi cha mwaka huu kwa kuwa inadhihirisha kuwa kampuni
inajali suala la usalama na afya kwa wafanyakazi na hili ni jambo la msingi kwa
kuwa usalama na Afya ukikosekana mazingira yetu ya kufanyia kazi yatakuwa
hatarini na ufanisi hautakuwepo”.Alisema.
Aliwapongeza wafanyakazi wote kwa jinsi
wanavyoshiriki kuzingatia kanuni na miongozo inayowekwa na kampuni hali
ambayo inachangia kuleta mafanikio na kuvifanya viwanda vilivyopo chini ya TBL
Group kuongoza kufanya vizuri na kuwa mfano wa kuigwa na viwanda vingine
nchini.
Kwa upande wake Meneja wa Usalama na Afya kwa
TBL,Renatus Nyanda,amesema kuwa kampuni imeweka mikakati kuhakikisha viwanda
vyake vyote vinatekeleza kanuni za Afya na Usalama kwa viwango vya kimataifa na
ndio maana inaendelea kupata tuzo hizi za Usalama kuazia zinazotolewa na
taasisi za hapa nchini na nje ya nchi “Leo tunaposheherekea kupata tuzo hii
wenzetu wa Mbeya nao wanasheherekea na ukaguzi unaendelea katika viwanda vingine”.Alisema
Alitoa wito kwa wafanyakazi wote wa viwanda vya
TBL Group kuendelea kutekeleza miongozo mbalimbali ya utendaji wenye kuleta
ufanisi ili waendelee kuwa kioo hususani katika suala hili la usalama na Afya
kwa kuwa linawagusa moja kwa moja katika maisha yao ya kila siku.
NOSA congratulates TBL on your achievement and recognises the work that TBL continues to do at improving workplace health and safety in Tanzania.
ReplyDeleteRegards Duncan Carlisle (CEO: NOSA)