August 08, 2016

VIFAA BORA NA VYA KISASA VINAPUNGUZA MATUKIO YA AJALI VIWANDANI

Meneja Ugawaji  wa huduma za TBL Group,James Nyoike,amesema kuwa   utumiaji wa vifaa bora na vya kisasa unapunguza matukio ya  ajali sehemu za kazi hususani  viwandani na kuongeza ufanisi wa kazi na kuongeza uzalishaji.


Bw.Nyoike aliyasema hayo wakati wa kupokea magari ya kupakia na kupakua  mizigo (Forklifts) za kisasa zilizonunuliwa na kampuni hiyo kutoka kampuni ya kusambaza vifaa vya viwandani ya Effco Solution Limited.

Alisema kampuni  ya TBL Group inao  makakati kuhakikisha inatumia mitambo ya kisasa na vifaa vya kisasa  kwa ajili ya kulinda usalama wa wafanyakazi wake ikiwemo kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji “Tunapoongelea vifaa vya kisasa hatumaanishi mitambo tu bali hata vifaa vyote vinavyotumika katika kazi ikiwemo magari yanaotumika kusambaza bidhaa zetu na yanaotumiwa na wafanyakazi wetu katika shughuli mbalimbali “.Alisema.  

Dereva akiendesha moja ya Forklift nne za kisasa zilizonuliwa na kampuni

Meneja Ugavi na Usambazaji  wa  TBL Group  ,James Nyoike ( wa  Nne kutoka kulia)  na madereva wa kuendesha Forklifts  wakimsikiliza  mtaalamu kutoka EFFCO Solution    Donald Luvaga (kushoto), jinsi Forklift za  kisasa aina ya Toyota zilizonunuliwa na kampuni ya TBL zinavyofanya kazi.



Mtaalamu kutoka EFFCO Solution, Donald Luvaga kitoa maelekezo kwa Madereva wa Forklift wa TBL Group.

No comments:

Post a Comment