SHIRIKA
la Umeme Tanzania, (TANESCO), linawaomba radhi wateja wake wa Mkoa wa Temeke,
kufuatia katizo la umeme usiku wa kuamkia leo Agosti 20, 2016.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Uhusiano Makao Makuu, sababu za kukatika
kwa umeme ni hitilafu iliyotokea kwenye njia ya umeme unaotoka Ilala kwenda
Kurasini, natayari mafundi wa TANESCO kutoka mkoa wa Temeke wanaendelea na kazi ya kurekebisha hitilafu hiyo.
Maeneo
yaliyoathirika na katizo hilo ni pamoja na Mbagala yote, Kurasini yote, Mtoni
yote, na baadhi ya maeneo ya Temeke.
Taarifa
hiyo imesema, baada yahitilafu hiyo mara moja mafundi wa TAENESCO waliingia
kazini usiku huo huo na hadi kufikia majira ya asubuhi, baadhi ya maeneo kama
vile Temeke, na Kurasini umeme ulirejea.
Taarifa
hiyo inasema, umeme utarejea katika hali yake ya kawaida kwenye maeneo yote muda
mfupi ujao na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Taarifa hiyo
imewataka wananchi kutoshika au kukanyaga waya wa umeme uliokatika au kuanguka
na pindi uonapo hali hiyo kwenye eneo lako, tafadhali wasiliana na TANESCO
kupitia namba zifuatazo, :Kituo cha miito ya simu namba 2194400 au 0768-985100.
Shirika linawaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu uliojitokeza.
No comments:
Post a Comment