August 27, 2016

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SH.3 BILIONI HALMASHAURI YA ARUSHA DC WILAYANI ARUMERU

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa akiwaongoza Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia(FFU)kuingia katika halmashauri ya wilaya ya Arusha DC baada ya kumaliza mbizo zake halmashauri ya wilaya ya Meru zote zikiwa katika wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha .
Kiongozi wa Mbio za Mwenge  kitaifa mwaka 2016,George Mbijima akivalishwa Skafu na kijana wa Scout wakati wa kuanza kukimbiza Mwenge wa Uhuru katika halmashauri ya wilaya ya Arusha DC.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijima akisalimiana na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha DC kabla ya kuanza kuweka Mawe ya Msingi na kuzindua miradi yenye thamani ya zaidi ya Sh 3 bilioni.
Mkurugenzi wa New Age Company Ltd,Godson Ngomuo akimwonyesha Samani zinazotengenezwa na kuuzwa na kampuni yake na kusaidia kutengeneza ajira kwa vijana wazawa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijimaakizungumza na maafisa wa taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wilaya ya Arumeru wanaotoa elimu dhidi ya Rushwa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijima  akijiandaa kukabidhi hundi yenye thamani ya Sh 3 milioni kwa kikundi cha Vijana waliopata mikopo yenye riba nafuu,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Alexander Mnyeti.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijima akiwakabidhi  hundi yenye thamani ya Sh 3 milioni kikundi cha Wanawake  waliopata mikopo yenye riba nafuu,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Alexander Mnyeti.
Vijana wa JKT Oljoro na Scout wakiserebuka kushangilia Mwenge wa Uhuru.
Moja ya mradi wa maji uliozinduliwa katika Kijiji cha Lekamba.

No comments:

Post a Comment