August 04, 2016

MANJANO FOUNDATION WAKUTANA NA WANAWAKE WA KUJADILI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI

Meneja Rasilimali watu Kutoka Benki ya NMB Dada  Edith Mwiyomela  akitoa Mada kwa Wanawake Wa Mkoa wa Dar es Salaam walionufaika na Mradi Kutoka Taasisi ya Manjano waliokutana kujadili na Kuangalia namna ya Kutatua changamoto wanazokutana nazo kwenye Biashara yao ya Upambaji na Uuzaji wa Vipodozi, Ambapo wameaswa Kuwafanya Kazi kwa Bidii,kuwa na Nidhamu na Pia kuweka akiba Pamoja na Kuwa na uvumilivu kwenye kazi zao za kila siku ili kuweza  Kufikia Malengo waliyojiwekea.  
Washiriki wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali kwenye mkutano huo
Afisa Mtendaji Mkuu wa wa Shear Illusions na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser (kushoto) Akimsiliza Mmoja wa Wanawake aliyekuwa akieleza namna anavyopambana na Changamoto zinzowakabili Wanawake wengi kwenye  Biashara zao.Kwa Upande Mwingine Mama Shekha Nasser Amawataka Wanawake  waliohudhuria namna gani ya kuweza kutofautisha faida na mtaji. Biashara nyingi za kina mama hufa baada ya mwaka mmoja tu kwa sababu wanawake wengi hawana nidhamu ya kutunza pesa. Hivyo tutaona matokeo ya 'Savings Club' zitakavyo wawezesha kusave pesa ili wasiweze kula mitaji na faida yote kwa pamoja
Washiriki wakisiliza kwa Makini Namna ya Kupambana Changamoto mBalimbali zilizowsilishwa kwenye Mkutano huo

No comments:

Post a Comment