Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na Balozi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shio (katikati) kulia ni Waziri Mambo ya Njena ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika
Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika umefanyika mchana huu katika
ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijianda na mkutano wa Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC Troika
Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini
mwa Afrika umefanyika mchana huu katika
ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.
Hii ndio muonekano wa Ukumbi wa Mkutano wa Mandvulo Grand uliopo Lozitha mjini Mbabane Swaziland ambapo mkutano wa 36 SADC unafanyika.
************
Mkutano wa Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika
Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika umefanyika mchana huu katika
ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.
Mkutano huo
wa Troika unaohusisha nchi Tatu ambazo ni za Utatu ikiwemo Tanzania, Msumbiji
na Afrika Kusini ambapo kwa kuzingatia utaratibu huo mkutano huo unahudhuriwa
na Wakuu wa nchi na serikali wa Msumbiji kama Mwenyekiti wa Asasi hiyo (SADC
Organ Troika Summit) na Afrika Kusini kama mwenyekiti aliyetoka na Tanzania
inatarajiwa kukabidhi uenyekiti wa Asasi hiyo.
Baadhi ya
ajenda ambazo viongozi hao watajadili kwenye mkutano huo ni hali ya ulinzi na
usalama katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar na Lesotho,
masuala ya upatanishi na utatuzi wa migogoro pamoja na maombi ya Burundi na
Comoro kutaka kujiunga katika Jumuiya ya Mandeleo Kusini mwa Afrika- SADC.
Katika
mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Ufunguzi
rasmi wa mkutano wa SADC utafanyika terehe 30-Aug-16 katika ukumbi wa Grand-
Lozitha mjini Mbababe Swaziland ambapo pamoja na Mambo mengine mkutano huo
utatoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda katika uandishi wa insha katika jumuiya
hiyo. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
No comments:
Post a Comment