KAMPENI ya mawakala wa kuuza vinywaji vya Kampuni ya Tanzania
Distilleriers Limited (TDL) inayojulikana kama “Nunua, Uza, Shinda na Konyagi ambayo
itawezesha washindi kujipatia malori ya usambazaji bidhaa inazidi kupamba moto.
Baadhi ya mawakala wa kampuni hiyo kutoka mikoa mbalimbali
wanaendelea na mikakati mizito ya usambazaji vinywaji ili kufikia lengo la
kuingia kwenye droo kila mmoja akiwa amepania kujishindia lori la zawadi ya
kampeni hii.
Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe, amesema kuwa
baada ya kukamilika zoezi la uzinduzi kila kanda ambao umekuwa na mafanikio na
kuwashirikisha mawakala wanaouza bidhaa za kampuni hivi sasa kazi kubwa imebaki
kwao kufanya mauzo na kufikia viwango vya kuingia kwenye droo ya kupata
washindi.
“Dhumuni kuu la kampuni yetu ya TDL kubuni kampeni hii ni
kuwainua wasambazaji wa biashara zetu. Tutaweza kufikia lengo hili kwani
washindi wawili katika kampeni hii watajishidia magari mapya mawili ya
usambazaji aina ya Eicher yenye uzito wa tani 3 pia tunazo zawadi
mbalimbali ambazo zimetengwa kwa ajili ya kuongeza motisha kwao katika kipindi
hiki cha kampeni”alisema.
Alisema kampeni itadumu kwa kipindi cha wiki 12 na wasambazaji
wanaoshiriki wamewekewa viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia
vigezo wataingia kwenye droo kubwa ya kupata mshindi mwezi Oktoba mwaka huu .
“Tunaamini kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao
watoongezea chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”.Alisema.
Baadhi ya mawakala wamepongeza jitihada za kampuni kutenga zawadi kubwa
za promosheni ambazo zitawawezesha washindi kurahisisha biashara zao badala ya
zawadi ndogondogo zisizoweza kumwinua kimaisha mshiriki.
Mmoja wa wauzaji wa bidhaa ya Konyagi kanda ya Ziwa aliyejitambulisha
kama John Masanja amesema kuwa japo sio mawakala wote watapata malori lakini
watakaobahatika kushinda watakuwa wamepata zawadi ya uhakika na inayofanikisha
biashara kukua.
“Kampeni hii ya Konyagi ni kubwa cha muhimu ni kukidhi vigezo
vya kuingia kwenye droo ya kumpata mshindi “.Alisema.
No comments:
Post a Comment