Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Utamaduni, Lily Beleko (katikati) kutoka Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizindua Kitabu cha Kamusi ya
Ukristo katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. kulia ni
Mhadhiri Chuo Kikuu Katoliki (WEA) Nairobi na Mhariri Mkuu wa Kampuni ya
Uchapishaji ya Gaba Publications , Padri, Dk.Jordan Nyenyembe ambaye
ndie mtunzi wa kitabu hicho na Padri Ubaldus Kidavuri
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni, Lily Beleko kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizungumza jambo kabla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Ukristo katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Publishers, Walter Bgoya akizungumza jambo kabla ya uzinduzi wa kitabu cha Ukristo
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dk. Selemani Sewangi akionesha kitabu hicho kwa wadau na kwa waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi huo wa kitabu cha Kamusi ya Ukristo kilicho zinduliwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni, Lily Beleko kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
***********
Na Khamis Mussa
SERIKALI inawashauri viongozi wa dini nchini kuendelea kutafsiri maneno magumu ya kidini ili kuepusha chuki, vurugu, ghasia na mapigano katika jamii.
Kauli hiyo
ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo ililisomwa na Kaimu Mkurungezi wa
Maendeleo ya Utamaduni, Lilly Beleko katika uzinduzi wa ‘Kamusi ya Ukristo’
jijini Dar es Salaam .
Alisema
kuzinduliwa kwa kamusi itahamasisha na kurahisisha uelewa wa vitabu na maandiko
kwa usahihi na ufasaha kwa jamii na kuleta upendo, Utulivu na Amani.
“Lugha yetu
ya Kiswahili ni chombo muhimu cha mawasiliano ambachokimekuwa kiungo cha
kuimarisha umoja, Amani na uzalendo, hivyo lazima tukiendeleze,” alisema.
Alisema
serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za
za kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili na kuthamini wanataaluma na wadau wa harakati za kutetea
hadhi ya Kiswahili.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Padre Abadius Kidavule
alisema ni mara ya kwanza Tanzania ndani ya Kanisa Katoliki kuzinduliwa Kamusi
ya Ukristo.
“Ni jambo
la kujivuni kuzindua kamusi, hivyo watanzania wanapaswa
kukinunua ili wajisomee,” alisema.
Mwandishi wa
Kanusi hiyo, Dk.Jordani N yenyembe alisema watanzania tumefanya makossa
kutopenda kusoma vitatu, hali imesabisha kupatikana waandishi wachache wa
vitatu.
No comments:
Post a Comment