Mkurugenzi
Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania ( ATE) Dk.Aggrey Mlimuka (wa pili
kulia ) akibadilishana mawazo na Meneja Vipaji wa TBL Group
Lilian Makau Galinoma (wa pili kushoto) wakati wa uzinduzi wa
mpango wa Mwanamke wa Wakati Ujao Tanzania ( Female Future
Tanzania) utakaoendeshwa na Chama cha waajiri Tanzania( ATE)
.Kushoto ni Meneja bidhaa wa Kiwanda cha Konyagi (DTL)Warda Kimaro
na Meneja Mkuu mpishi wa pombe wa Chibuku.(DARBREW) Neema
Arora. Uzinduzi umefanyika katika hoteli ya Sea
Cliff jijini Dar es Salaam
Meneja wa kuendeleza Vipaji wa TBL Group Lilian Makau Galinoma
akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mpango wa Mwanamke wa
wakati ujao Tanzania ( Female Future Tanzania) ulioanzishwa na na
Chama Cha waajiri Tanzania( ATE) .Uzinduzi ulifanyika katika iliyofanyika
hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania ( ATE) Dk.Aggrey
Mlimuka (kulia) akimpongeza Meneja wa kuendeleza Vipaji wa TBL
Group Lilian Makau Galinoma mara baada ya kumaliza kutoa mada wakati wa
uzinduzi wa Progamu ya Mwanamke wa wakati ujao Tanzania (
Female Future Tanzania) iliyoandaliwa na Chama cha waajili Tanzania( ATE)
katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Watendaji waandamizi wa taasisi mbalimbali wakiw wakifuatilia mada
wakati wa uzinduzi wa mpango wa Mwanamke wa wakati ujao Tanzania (
Female Future Tanzania) wakati wa uzinduzi wake katika hoteli ya Sea
Cliff jijini Dar es Salaam
Watendaji
waandamizi wa taasisi mbalimbali wakiwa katika picha ya washiriki wa mpango wa
Mwanamke wa wakati ujao Tanzania ( Female Future Tanzania)
wakati wa uzinduzi wake katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar
es Salaam.
**************
WANAWAKE watatu kutoka kampuni ya TBL Group wamechaguliwa kujiunga na
mpango wa mwanamke wa wakati ujao ambao imeanzishwa na Chama Cha Waajiri
Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri nchini
Norway ambao umeenga kuboresha ufanisi wa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi
hapa nchini.
Mpango huu ambao umezinduliwa jijini Dar es Salaam unawashirikisha
wanawake wapatao 33 kutoka makampuni mbalimbali nchini ambao watapatiwa mafunzo
mbalimbali ya uongozi.
Akiongea kwa niaba ya wenzake Meneja wa kuendeleza vipaji wa TBL Group
Lilian Makau Galinoma ambaye amechaguliwa kushiriki katika mpango huu
alisema wanashukuru kampuni yao kwa kuona umuhimu wa kuendeleza
wafanyakazi wake.
“Tunaishukuru kampuni yetu kwa kutufadhili ili tuweze kupata mafunzo ya
uongozi na tuna imani yatatupa upeo zaidi wa kuboresha utendaji wa kazi zetu za
kila siku ikiwemo kuendeleza vipaji vya wafanyakazi wenzetu wa kike
“.Alisema.
No comments:
Post a Comment