Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, George Lugomela akitoa hotuba kwa niaba ya serikali katika kongamano hilo. (Picha na Modewjiblog)
Mshauri Mwandamizi wa UNESCO, Bruno Nguyen, akielezea umuhimu wa kongamano hilo.
Mtaalam wa programu wa UNESCO, Alexandros Makarigakis akitoa takwamu za usalama wa maji na jinsi taka mwili za binadamu zinavyoyafanya maji yasiwe salama.
***********
Katika
kuhakikisha kunakuwa na usalama wa maji duniani kutokana na kuwepo kwa
idadi kubwa ya vifo ambavyo vinatokana na uchafu katika maji, Shirika la
Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
limefanya kongamano la siku moja ambalo limewakutanisha viongozi wa
idara za maji za mikoa mbalimbali nchini na kutoka nje ya nchi.
Katika
kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali
za Maji kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, George Lugomela alisema
sehemu kubwa ya vyanzo vya maji zimekuwa vikichafuliwa kutokana na usafi
wa binadamu. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Alisema
kuwa takwimu zinaonyesha ni asilimia 24 ya watu Afrika ndiyo
wanajisaidia katika maeneo ambayo ni salama na idadi iliyobakia wamekuwa
wakijisaidia mazingira ambayo yanahatarisha vyanzo vya maji na wengi
wao wakijisaidia maporini.
"Kongamano
hili linaangalia kuhusu vijidudu vilivyo katika maji ambavyo kwa
asilimia kubwa yanachafuka kutokana na usafi ambao anaufanya binadamu na
ukiangalia kwa nchi zetu inaonyesha bado uhifadhi wa hizo taka kama
kinyesi ambacho baadae huathiri vyanzo vya maji ni mdogo," alisema
Lugomela.
Aidha
alisema pamoja na maeneo mengine kufanya ujenzi wa vyoo lakini jambo
hilo bado sio salama kwa asilimia 100 na hivyo inahitajika kufanyika
jitihada za ziada ili kuweza kuviweka vyanzo vya maji katika hali ya
usalama.
Nae
Mshauri Mwandamizi wa UNESCO, Bruno Nguyen, alisema kuwa kongamano hilo
lina malengo ya kupata suluhisho ili kuhakikisha watu ambao wanaishi
bara la Afrika wanapata maji safi na salama.
Katika
ripoti ya mwaka 2014 ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya (WHO)
inaonyesha kuwa watu bilioni 1.8 duniani kote wanatumia maji ambayo yana
vijidudu.
Baadhi ya watu waliohudhuria kongamano hilo la siku moja kutoka mikoa mbalimbali na nchi jirani.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment