July 26, 2016

TBL GROUP YADHAMINI SEMINA YA WAKAGUZI WA MAGARI WA POLISI MWANZA

 Wakaguzi wa magari kutoka jeshi la Polisi wakifuatilia mafunzo wakati wa semina ya ukaguzi wa magari iliyofanika jijini Mwanza
 Wakaguzi wa magari kutoka jeshi la Polisi wakifuatilia mafunzo wakati wa semina ya ukaguzi wa magari iliyofanika jijini Mwanza
 Wakaguzi wa magari kutoka jeshi la Polisi wakifuatilia mafunzo  ya ukaguzi wa magari kwa vitendo kutoka kwa Mkufunzi Hubert Kubo kutoka kampuni ya CFAO wakati wa semina ya ukaguzi wa magari iliyofanyika jijini Mwanza.
 Wakaguzi wa magari kutoka jeshi la Polisi walitembelea maeneo ya kiwanda.
 Wakaguzi wa magari kutoka jeshi la Polisi  wakishauriana jinsi ya ukaguzi wa magari makubwa wakati wa semina hiyo.
Wakaguzi wa magari kutoka jeshi la Polisi  wakishauriana jinsi ya ukaguzi wa magari makubwa wakati wa semina hiyo.
*************
KATIKA mkakati wake wa  kushirikiana na serikali na jamii katika kutoa elimu ya usalama, kampuni ya TBL Group imedhamini semina kwa  wakaguzi wa magari kutoka Jeshi la Polisi jijini Mwanza ambayo imefanyika katika kiwanda cha TBL cha Mwanza na kuendeshwa na Mtaalamu wa magari kutoka kampuni ya CFAO,Bw.Hubert Kubo.

Semina hiyo iliendeshwa kwa  njia shirikishi ambapo  washiriki walijadiliana masuala mbalimbali yanayohusiana na usalama barabarani na changamoto zilizopo katika kukagua vyombo vya moto na  jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini.

No comments:

Post a Comment