July 03, 2016

SERIKALI YAUPONGEZA MFUKO WA PENSHENI WA PPF

 WAZIRI wa  nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, na tuzo waliyotwaa ya ushindi wa kwanza kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Makampuni ya Bima kwenye maonesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaa, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 2, 2016. Waziri aliupongeza Mfuko huo kwa kuibuka mshindi wa kwanza kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Makampuni ya Bima na kuitaka mifuko mingine kufanya juhudi ili kufikia mafanikio hayo.

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akimkabidhi Vumilia Joseph Twigela,  kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,  kupitia mfumo maalum wa kuchangia unaohusisha watu wote wenye kipato, ujulikanao kama Wote Scheme, wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.
 WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, ameupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF, kwa kupata tuzo ya mshindi wa kwanza kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Makampuni ya Bima, kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dares Salaam.
*****************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, ameupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF, kwa kupata tuzo ya mshindi wa kwanza kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Makampuni ya Bima, kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dares Salaam.

Waziri alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea banda la PPF mwishoni mwa wiki ambapo alitoa changamoto kwa Mifuko mingine kufanya juhudi ili kufikia mafanikio ambayo PPF imeyapata.
Waziri Mhagama ambaye alikuwa akitembelea Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo iko chini ya Wizara yake inayoshiriki maonyesho hayo, alishuhudia wafanyakazi wa Mfuko huo wakitoa huduma mbalimbali kwa wananchi waliofika kutembelea banda hilo ambapo miongoni mwa kazi alizofanya Waziri Mhagama, ni kumkabidhi kadi mpya ya uanachama, Vumilia Joseph Twigela, ambaye yeye pamoja na mfanyakazi wake wa ndani walijiunga na mfumo maalum wa kuchangia unaohusisha watu wote wenye kipato, ujulikanao kama Wote Scheme.
“Ninawapongeza kwa kuibuka kidedea mbele ya Mifuko mingine, na nitoe wito kwa wengine kufanya juhudi ili kufikia mafanikio yenu.” Alisema Waziri Mhagama ambaye alifuatana na Maafisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, alitembelea idara ya uendeshaji ambayo inahusika na utoaji elimu na kujiunga na uanachama.

Pia alitembelea idara ya Michango ya wanachama ambapo Waziri alipewa maelezo ya kina kuhusu huduma zitolewazo na wafanyakazi wa PPF kwa wanachama wanaofika kupatiwa huduma.
Hali kadhalika Waziri Mhagama alitembelea kurugenzi ya uwekezaji na kuupongeza Mfuko huo kwa kuanza kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais ambaye alitaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuwekeza kwenye viwanda ili kutengeneza ajira zaidi na kupata wanachama wengi.

No comments:

Post a Comment