Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) akikabidhi msaada
wa mashine ya kutengeneza sabuni na vifungashio vyenye thamani ya zaidi ya
milioni 10/- kupitia mpango wa Airtel FURSA ‘Tunakuwezesha’ kwa Mwenyekiti wa Kikundi
cha Tupendane cha Tandika, Nasra Haji katika hafla iliyofanyika kituoni hapo Manispaa
ya Temeke jijini Dar es Salaam jana. Kushoto
ni Afisa Maendeleo ya Vijana wa Manispaa hiyo, Anna Marika.
Afisa Maendeleo ya Vijana wa Manispaa ya Temeke, Anna Marika (kushoto)
akikabidhi kwa niaba ya Airtel msaada wa na vifungashio vya sabuni baada ya kampuni hiyo kukabidhi mashine ya kutengeneza sabuni vyenye thamani
ya zaidi ya milioni 10/- kupitia mpango wa Airtel FURSA ‘Tunakuwezesha’ kwa
Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Tandika, Nasra Haji katika hafla iliyofanyika kituoni hapo jijini
Dar es Salaam jana. Wa (pili kushoto) ni
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
Afisa Maendeleo ya Vijana wa Manispaa ya Temeke, Anna Marika (kushoto)
akikabidhi kwa niaba ya Airtel msaada wa na vifungashio vya sabuni baada ya kampuni hiyo kukabidhi mashine ya kutengeneza sabuni vyenye thamani
ya zaidi ya milioni 10/- kupitia mpango wa Airtel FURSA ‘Tunakuwezesha’ kwa
Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Tandika, Nasra Haji katika hafla iliyofanyika kituoni hapo jijini
Dar es Salaam jana. Wa (pili kushoto) ni
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
************
Kufatia mchango wake katika
maendeleo ya miradi ya vijana Serikali imeupongeza mpango wa Airtel FURSA kwa
kuwawezesha vijana nchi nzima kukuza uchumi wao.
Hayo yamesemwa na Afisa maendeleo ya
vijana wa wilaya ya Temeke , Bi Anna Marica wakati Airtel kupitia mpango wake
wa Airtel FURSA ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa
kikundi kilichoundwa na wanawake 12 cha Tupendane kilichopo Temeke jijini Dar
es salaam
Alisema” kupitia mradi wa
Aritel FURSA, Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana
nchini na kupongeza kikundi cha Tupendane kwa kuwa moja kati ya vikundi
vilivyofikiwa na Airtel FURSA
“Kikundi cha Tupendane kimeonyesha
mfano mzuri hususani kwa vijana wakike na napenda kuwahasa muongeze hari na
kufanyakazi kwa bidii zaidi ili kuongeza uzalishaji na kutengeneza ajira kwa
vijana waishio jijini Dar es salaam.” Alisema Marica
Msaada wa vifaa uliotolewa kwa
kikundi hicho ni pamoja na mashine mpya ya kutengenezea sabuni, vifungashio
pamoja na kuboreshewa mazingira ya ofisi ya kufanyia kazi.
Kwa upande wake Meneja huduma kwa
jamii, Bi Hawa Bayumi alisema“ tunatambua juhudi na ubunifu mkubwa
unaofanywa na kikundi hiki na tunaamini msaada huu utasaidia kuinua mapato
yao kwa ujumla.
“Huu ni msimu wa pili wa mradi
wetu wa Airtel FURSA ambapo mpaka sasa tumeweza kuwafikia vijana wajasiriamali
20, makundi ya wajasiriamali 30 pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa
zaidi ya vijana 3000 nchini. leo tunajisikia furaha kukiwezesha kikundi hiki
cha Tupendane kwani tunatambua kwa kuwawezesha vijana hawa 12 tutaweza
kuziwezesha familia zao na jamii kiuchumi kwa namna moja au nyingine“ alisema
Bayumi
Mwenyekiti wa kikundi cha Tupendane
Nasa Hija Siri aliwashukuru Airtel kwa kuwafikia vijana wengi na kutatua
changamoto zao na kuahidi kutumia msaada huo kuongeza uzalishaji
“ kupitia msaada huu
tunauhakika wa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa bidhaa zetu kwani kwa sasa
tunatengeneza lita 20 kwa siku, na kwa msaada huu sasa tutazalisha hadi lita
100 kwa siku haya kwetu sisi ni mafanikio makubwa na tunawashukuru sana
Airtel”alisema Nasa
Kikundi cha tupendane kilianza
biashara zake kwa kuuza vitenge na kukopesa kwa wateja, biashara hii haikuwa ya
mafanikio kwani wateja walishindwa kulipa madeni yao kwa wakati ndipo
walipoamua kuanzisha biashara ya kutengeneza na kusambaza sabuni za maji na
shampoo za nywele
No comments:
Post a Comment