Sabuni mara nyingi tumezoea kuziona zikitengenezwa na viwanda vikubwa nchini na kupakiwa katika maboksi nadhifu. Lakini kumbe kila mtu anaweza kuwa na kiwanda kidogo cha kuzalisha sabuni nyumbani kwake na kuwauzia majirani zake na kujipatia kipato yeye na familia yake baada ya kupata ujuzi maalum kutoka kwa watalaam.
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) ni mingoni mwa mashirika na taasisi ambaz zimekuwa zikiwafundishwa wananchi mbalimbali juu ya kuendesha viwanda vidogo na kufanya kazi za mikono pamja na usindikaji kutyokana na malighafi ambazo zinapatikana katika maeneo yao.
Akina mama wa Kigoma ni mingoni mwa waliopata ujuzi huo na sasa wao wanazalisha sabuni zitkanazo nazo nambeki za michikichi ambazo hubaki baada ya kukamuliwa mafuta.
Katika baadhi ya mitaa mjini Kigoma ukipita huwezi kukosa aina hii ya sababuni ikiuzwa kwa wingi. Wauzaji wake ni akina mama na watoto ambao husaidia wazazi hao kufanya bishara hiyo.
Bei ya mche mmoja wa sababuni hii ni Sh 1,000. Uzalishaji wa sabuni hizo kutkana na bidhaa za michikichi nao umengeza pato la wakuliwa wa Michikichi ambao awali walikuwa wakitegemea zaidi kutkana na mafuta yake.
Mbali na mkoani Kigoma lakini Sababuni hizi hivi sasa zinapatikana katika maeneo mengi nchini. Dar es Salaam napo zipo, na mikoa mingine jirani na Kigoma kama Kagera napo zinapatikana.
Sabuni hizi zina majina mawili ya MZAZI na BORA. Hayo ni majina ya mihuri tu lakini si kuwa zinazalishwa na watru wawili bali kila mtu huzalisha kivyake na kupiga muhuri hiyo.
Akina mama hawa na watoto hujipatia kipato kutokana na biashara hii na kuweza kusaidia kukuza pato la familia licha ya changamoto za soko la uhakika kwa wajasiriamali hawa ndio kikwaz kikubwa.
No comments:
Post a Comment