Meneja
Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena (wa pili kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani moja ya majarida ya utalii ya TTB yaliyopo
katika Banda la TTB.
Kaimu
Mkurugenzi wa Masoko wa TTB Bw. Philip Chitaunga(wa pili kulia ) akitoa maelezo
kuhusu namna tuvuti maalumu ya Utalii (Online Tourism Portal) inavyofanya kazi na inavyoweza
kutumiwa na wadau wa utalii kwa Naibu Waziri Maliasili na Utalii Eng. Ramo
Makani huku afisa wa TTB Bw.Francis Malugu akisaidia kuonyesha kurasa za tovuti
hiyo .
Naibu
Waziri Eng. Ramo Makani akisisitiza jambo kuhusu tovuti maalumu ya Utalii baada
ya kupata maelezo kuhusu tovuti hiyo kutoka kwa maafisa wa TTB.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani ameipongeza Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) kwa kazi nzuri inayoifanya katika kuitangaza Tanzania kama eneo
bora la Utalii Duniani kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo tovuti maalumu ya
utalii (Online Tourism Portal) na Nyenzo maalumu ya kutangaza utalii wa
tanzania kupitia simu za mkononi ( Tanzania Tourism App).
Naibu
Waziri huyo ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la Bodi ya Utalii Tanzania
lililopo ndani ya jingo la Wizara ya Maliasili na Utalii katika viwanja vya
Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
“
Kwa hakika mnafanya kazi nzuri sana katika kutangaza vivutio vyetu vya utalii,
endeleeni na juhudi hizo” alisema Naibu Waziri mara baada ya kupata maelezo
mafupi kuhusu mbinu zinazotumiwa na TTB katika kuitangaza Tanzania kama eneo
Bora la Utalii Duniani.
No comments:
Post a Comment