Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde akizungumza katika kongamano la Vijana jijini Mwanza hii leo. Kongamano hilo limewakutanisha vijana zaidi ya 1,000 kutoka katika Wilaya zote za mkoa wa Mwanza.
Mavunde amewataka vijana kuthubutu na kutokatishwa tamaa katika kufanya uwekezaji huku wakitambua kwamba taifa hili linawategemea.
Pia nimesisitiza vijana kufanya kazi na kuacha kutumia muda mwingi kufanya shughuli ambazo hazina tija.
Aidha Naibu Waziri Mavunde, amesisitiza kwamba serikali itaendelea kutenga maeneo maalum ili kuwezesha vijana kushiriki katika shughuli za uchumi.
Kongamano hilo liliwakutanisha vijana wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali kupitia miradi ya Kilimo, Ufugaji, Uvuvi na waliowekeza katika viwanda vidogo vidogo.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde akizungumza katika kongamano la Vijana jijini Mwanza hii leo.
Vijana zaidi ya takribani 1,100 walikutana pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo mkoani humo na nchini kwa ujumla.
Vijana hao pia walijadili namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi zinazowakabili vijana wa Mwanza na namna ya kutumia rasilimali zilizopo mkoani humo kujikwamua kiuchumi.
Naibu Waziri Anthon Mavunde akijadiliana jambo na viongozi meza kuu.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde akiagana na vijana walioshiriki katika kongamano la Vijana jijini Mwanza leo.
No comments:
Post a Comment